Pamoja na Hadithi Tukufu
Kati ya Ukafiri na Imani ni Kuacha Swala
Tunawasalimu nyote wapendwa mahali popote mlipo, katika kipindi kipya cha kipindi chenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imetuhadithia Qutaiba akasema: Ametuhadithia Jarir, na Abu Muawiya, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abu Sufyan, kutoka kwa Jabir, kwamba Mtume, swallallahu alayhi wasallam, amesema: "Kati ya ukafiri na imani ni kuacha swala" Jamiu Tirmidhi 2663
Hakika hadithi hii inafafanua na kubainisha mstari unaotenganisha kati ya ukafiri na imani, yaani mstari unaotenganisha kati ya kinzani mbili, ukafiri na imani. Basi kinachotenganisha jambo hili ni swala, na jambo hili ni kinaya ya ibada na kushikamana na hukumu za kipekee na za jumla, kwa hivyo ikiwa itachukuliwa kwa maana ya lugha basi itakuwa ni kufanya ibada za kipekee zinazohusiana na uhusiano wa Muislamu na Mola wake, basi inampasa kudhihirisha kwamba anashikamana na kile kinachomkurubisha mja kwa Mola wake, na anafanya amali ambazo Mwenyezi Mungu amemfaradhishia, za kufanya vitendo ambavyo vinadhihirisha shukrani, ibada na kujikurubisha kwake, na kilele chake ni swala, na ikiwa jambo hili litachukuliwa kwa maana ya jumla nalo ni kutaja kitu na kukusudia hukumu; Na jambo hili lina uwezekano katika maandishi; Kwa kuwa swala ni kinaya ya hukumu ambazo Mwenyezi Mungu amezisharia kwa mwanadamu, basi inampasa mtu asitosheke na kusema kwa imani, bali inampasa afuate matendo yanayoendana na imani, nayo ni kutekeleza hukumu ambazo imani imeleta na Mwenyezi Mungu ametutaka. Na kwa msingi huu, maandishi haya yanaeleweka kwa mambo mawili na yote ni sahihi, na kwa msingi huo inatupasa sisi Waislamu kushikamana na hukumu za kipekee za ibada na miamala sawa, na hailingani kusadikisha kwa yakini Mwenyezi Mungu na kutotenda kivitendo usadikishaji huu, nayo ni utekelezaji wa hukumu ambazo Mwenyezi Mungu ameleta.
Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie kuwa miongoni mwa wale wanaoamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola na wanaendelea na imani kwa kushikamana kikamilifu kama ilivyokuja katika sheria juu ya nafsi zetu, na atufishe hali ya kuwa Waislamu, Ee Mwenyezi Mungu Amina.
Ee Mwenyezi Mungu, tuharakishie ukhalifa ulioongoka juu ya manhaji ya utume, ambao ndani yake utakusanya matatizo ya Waislamu, uondoe kwao yale waliyomo ya balaa, Ee Mwenyezi Mungu, nurisha ardhi kwa nuru ya uso wako mtukufu. Ee Mwenyezi Mungu, Amina Amina.
Wapendwa wetu, na mpaka tukutane tena na hadithi nyingine ya Nabii, tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu, na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imeandikwa kwa ajili ya redio na: Dkt. Maher Saleh