Pamoja na Hadithi Tukufu
Muacheni Mateka
Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali katika kipindi kipya cha programu yenu Pamoja na Hadithi Tukufu na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,
KUTOKA ABUU MUSA RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE AMESEMA: AMESEMA MTUME WA ALLAH SALLA ALLAHU ALAYHI WA SALAM: "MUACHENI MATEKA YAANI MFUNGWA NA MLISHENI MWENYE NJAA NA MTEMBELEENI MGONJWA"
Fath Al-Bari Sharh Sahih Al-Bukhari
"MUACHENI MATEKA" YAANI MFUNGWA.
AMESEMA IBN BATTAL: KUMUACHILIA MFUNGWA NI WAJIBU WA KIFAYA, NA HII NDIO KAULI YA JAMHURI. NA AMESEMA IS-HAAQ BIN RAHWAYH: KUTOKA BAITUL MAL. NA IMERIPOTIWA KUTOKA KWA MALIK PIA NA AMESEMA AHMAD ANAKOMBOLEWA KWA WAKUU, AMA KWA MALI SIJUI. NA IKIWA WAISLAMU WANA MATEKA NA WASHIRIKINA WANA MATEKA NA WAKAKUBALIANA KUACHILIANA, INALAZIMU, NA HAIRUHUSIWI KUWACHILIA HURU MATEKA WA WASHIRIKINA KWA MALI
Wasikilizaji wetu wapenzi:
Sote tunajua asili ya fiqhi ya hadithi hii ambayo Mtume wetu Mtukufu, Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam, anatuhimiza kumwachilia huru mateka, kulisha mwenye njaa, na kumtembelea mgonjwa. Lakini, niliwaza wazo linalotokana na uhalisia wa umma wa Kiislamu kwamba umma wa Kiislamu leo umetekwa, una njaa na unaumwa. Umetekwa kwa sababu ya utawala wa mifumo ya ukafiri juu yake kijeshi, kisiasa, kiuchumi, kiitikadi na kimawasiliano. Na una njaa kwa sababu baraka zake ambazo Mungu amemruzuku zimeporwa na baraka hizi zimekuwa bidhaa kwa kafiri anazifurahia. Na unaumwa kwa sababu ugonjwa wa ubepari umeenea mwilini mwake. Je, tutafanya kazi ya kuukomboa umma wa Kiislamu kutokana na utumwa, njaa na ugonjwa uliomo? Na hatuishii hapa, bali tunafanya kazi ya kuukomboa ulimwengu baada ya kujikomboa wenyewe?!
Wasikilizaji wetu wapenzi, mpaka tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya kinabii, tunawaacha katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.