Pamoja na Hadithi Tukufu
Haki ya Mwenyezi Mungu kwa Waja
Tunawasalimu nyote wapenzi wetu popote mlipo, katika kipindi kipya cha kipindi chenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, basi Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imetuhadithia Mahmud bin Ghailan, akasema: Ametuhadithia Abu Ahmad, akasema: Ametuhadithia Sufyan, kutoka kwa Abi Ishaq, kutoka kwa Amru bin Maimun, kutoka kwa Muadh bin Jabal, akasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alaihi wasallam: "Je, unajua haki ya Mwenyezi Mungu kwa waja?" Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi. Akasema: "Hakika haki yake juu yao ni wamwabudu na wala wasimshirikishe na chochote." Akasema: Je, unajua haki yao kwake wakifanya hivyo? Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi. Akasema: "Hatawaadhibu." Jaamiut-Tirmidhi 2690
Hakika hadithi hii tukufu inatueleza haki mbili kubwa, ya kwanza ni haki ya Mwenyezi Mungu kwa waja na haki ya pili ni haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu. Katika hadithi hii kuna maelezo kwa usahihi kabisa na kwa kina kuhusu haki, haki ya kwanza ni wazi kwa wote, na ametueleza Mwenyezi Mungu kupitia ulimi wa Nabii wetu, na ametueleza kwamba Mwenyezi Mungu amezifunga haki mbili pamoja, ya kwanza ni kwamba tumwabudu Mwenyezi Mungu na tusifanye pamoja na imani na ibada yoyote anayemshirikisha Mwenyezi Mungu katika haki hii, na jambo hili linafanywa kwa utekelezaji wa kweli wa hukumu za kisheria kama alivyoamrisha na kutufaradhishia, na kuamini kwa yakini Mwenyezi Mungu kwamba yeye ndiye Muumbaji, na hakuna anayestahili kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye, na hii ndiyo sehemu ya kwanza ya sharti au mkataba ambao Mwenyezi Mungu ameweka baina yetu na baina yake.
Na ama sehemu nyingine ya sharti ni kwamba Mwenyezi Mungu ameahidi kwamba hatatuadhibu wala hatoingiza motoni, na hii ni haki ambayo Mwenyezi Mungu ameweka juu ya nafsi yake, hivyo inavyoonekana ni kwamba masharti haya mawili yameambatana hayawezi kutenganishwa, na ni rehema kutoka kwa rehema za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, hivyo tunapaswa kuyahudhurisha masharti haya mawili daima, katika jambo la kwanza la kulifanya kama anavyopenda Mwenyezi Mungu subhanahu wa ta'ala, na matokeo ambayo hakuna shaka ndani yake ni kuingia peponi na kuachana na adhabu.
Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu atufanye miongoni mwa wale ambao wanashikamana na amri ya Mwenyezi Mungu na wala hatumshirikishi na yeyote, na tuwe miongoni mwa wale ambao wanastahiki kuachana na adhabu, Ewe Mwenyezi Mungu, amina.
Ewe Mwenyezi Mungu, tuharakishie ukhalifa ulioongoka juu ya manhaji ya utume ambao ndani yake unakusanya yaliyotawanyika ya Waislamu, uwaondolee yale ambayo wamo ndani yake katika balaa, Ewe Mwenyezi Mungu, nurisha ardhi kwa nuru ya uso wako mtukufu. Ewe Mwenyezi Mungu, amina amina.
Wapendwa wetu, na mpaka pale tutakapokutana na hadithi nyingine ya kinabii, tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu, na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Aliyeiandika kwa ajili ya redio: Dkt. Maher Saleh