Pamoja na Hadithi Tukufu - LAU MNGEKUWA KAMA MNNAVYOKUWA KWANGU
Pamoja na Hadithi Tukufu - LAU MNGEKUWA KAMA MNNAVYOKUWA KWANGU

2- Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali katika kipindi kipya cha programu yenu Pamoja na Hadithi Tukufu na tunaanza na salamu bora, basi Amani iwe juu yenu na Rehema za Mungu na Baraka zake,

0:00 0:00
Speed:
June 26, 2025

Pamoja na Hadithi Tukufu - LAU MNGEKUWA KAMA MNNAVYOKUWA KWANGU

Pamoja na Hadithi Tukufu

LAU MNGEKUWA KAMA MNNAVYOKUWA KWANGU

2- Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali katika kipindi kipya cha programu yenu Pamoja na Hadithi Tukufu na tunaanza na salamu bora, basi Amani iwe juu yenu na Rehema za Mungu na Baraka zake.

Kutoka kwa Hanzala Al-Katibu At-Tamimiyy Al-Usaidi alisema:

Tulikuwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimshukie, tukataja Pepo na Moto hata kama tulikuwa tunaona kwa macho, nikaenda kwa familia yangu na watoto wangu nikacheka na kucheza. Akasema: Nikakumbuka yale tuliyokuwa tukizungumzia, nikatoka nikakutana na Abu Bakr, nikasema: Nimefanya unafiki, nimefanya unafiki, Abu Bakr akasema: Hakika tunafanya hivyo. Hanzala akaenda na kumuelezea Mtume, rehema na amani zimshukie, akasema: "Ewe Hanzala, lau mngekuwa kama mnavyokuwa kwangu, malaika wangewasalimu kwenye matandiko yenu au kwenye njia zenu, ewe Hanzala saa na saa"

Imekuja katika maelezo ya Sunan Ibn Majah ya As-Sindi

Kauli yake (nimefanya unafiki) yaani hali yangu imebadilika kiasi kwamba haifai kupuuzwa kwa anayeziamini, basi kuzipuuza kunafanana na kuwa ni miongoni mwa kukana kwa siri uwepo wake na kwa ujumla, basi uwepo wa imani kwazo umemchanganya moyoni mwake bila shaka na akahesabu kuwa ni unafiki na kwa hili imedhihirika kuwa shaka katika imani haikufurishi, bali shaka katika anayeaminiwa ndio inayokufurisha

Kauli yake (lau mngekuwa kama mnavyokuwa)

Amewatahadharisha kuwa kuhudhuria hakudumu kawaida na kutokuhudhuria hakudhuru kuwepo kwa imani moyoni na kupuuza kunapingana na kuhudhuria basi haihitajiki kutokana nako kutokuwepo kwa imani; saa kunakuwa kuhudhuria ili jambo la dini litawalike kwalo na saa kunakuwa kupuuza ili jambo la dini na maisha litawalike kwalo na katika kila moja kati ya hayo kuna rehema kwa waja.

Wasikilizaji wetu wapenzi:

Hadithi Tukufu ambayo iko mikononi mwetu inathibitisha mambo kadhaa, ikiwemo:

Kwanza: Kwamba dhana ya (saa na saa) haina uhusiano wowote, wala wa karibu wala wa mbali na kile ambacho baadhi wanaelewa kuwa ni saa yako na saa ya Mola wako. Imefahamika kuwa maisha ya Muislamu yote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama alivyosema Mtukufu akifundisha waja wake waseme (Sema: Hakika sala yangu na ibada zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu)

Hakuna kitu katika maisha ya Muislamu kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu (amenunua kutoka kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao wanastahiki Pepo) basi Waislamu wote wameuza yote wanayoyamiliki kwa bei ya Pepo, naam, inaweza kuwa katika maisha ya Muislamu saa ya kuamka na saa ya kupuuza, na saa ya nguvu na saa ya udhaifu, na saa ya ukaribu na saa ya umbali, lakini haraka anakumbuka na anafahamu; basi anasukuma kupuuza na anaongeza nguvu udhaifu, na anakimbilia kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akasema: (Hakika wale wamchao Mungu wanapoguswa na wasiwasi kutoka kwa shetani hukumbuka, mara huona)

Na imekuja katika Hadithi Tukufu: (Kila mwana wa Adamu ni mkosaji na mbora wa wakosaji ni wenye kutubu)

Pili: Kwamba mawaidha na ushauri hautoshi pekee kuwa njia katika kujenga haiba na kubadilisha tabia. Pepo na Moto na kuogopesha na kutamanisha vyote ni miongoni mwa Uislamu. Lakini inapaswa kwamba wanazuoni wetu na wabebaji wa ulinganiaji wasipuuze pia kuwa hakuna budi pia na fikra na dhana za Kiislamu ambazo kila Muislamu anazihitaji katika maisha yake ya kila siku na ambazo zinaathiri tabia yake athari yenye kuleta matunda na iliyozingatia. Kwa Muislamu pamoja na ufahamu wake juu ya neema za Pepo na adhabu ya Akhera, anapaswa kufahamu kwa mfano ukweli wa mapambano kati ya Uislamu na Ukafiri na afahamu ukweli wa demokrasia na ulaikini na ubepari na afahamu ukweli wa itikadi ya Kiislamu kwa kuwa ni itikadi ya kiroho na kisiasa na afahamu kuwa Uislamu umekuja kutekelezwa na afahamu kwamba hakuna utekelezaji wa Uislamu isipokuwa kwa dola na afahamu sababu za kuchelewa kwetu na njia ya kuinuka kwetu.

Mwenyezi Mungu amesema:

(Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na wale walio pamoja naye ni wakali kwa makafiri, wenye huruma baina yao, utawaona wanarukuu, wanasujudu, wanatafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi, alama zao ziko katika nyuso zao kutokana na athari ya kusujudu, hiyo ndiyo mfano wao katika Taurati na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya shina lake, unawapendeza wakulima ili awakasirishe nao makafiri, Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini na wakatenda mema miongoni mwao msamaha na ujira mkuu)

Na Mwenyezi Mungu amesema: (Kueni watawa kwa sababu ya kuwa mlikuwa mnafundisha Kitabu na kwa sababu ya kuwa mlikuwa mnasoma)

Wasikilizaji wetu wapenzi na mpaka tutakapokutana na hadithi nyingine ya kinabii tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu na Amani iwe juu yenu na Rehema za Mungu na Baraka zake.

More from Sheria

Pamoja na Hadithi Tukufu - Je, mnajua ni nani mfilisi?

Pamoja na Hadithi Tukufu

Je, mnajua ni nani mfilisi?

Karibuni wasikilizaji wetu wapendwa, wasikilizaji wa redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir. Tunakutana nanyi tena na kipindi chetu pamoja na Hadithi Tukufu, na bora tuanzie nayo kipindi chetu ni salamu ya Kiislamu, basi Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imekuja katika Musnad Ahmad - sehemu iliyobaki ya Musnad ya Al-Mukthirin - Hakika mfilisi katika umma wangu ni yule anayekuja Siku ya Kiyama na funga na swala na zaka, na anakuja hali amemtukana huyu, amemsingizia huyu, na amekula mali ya huyu 

  Ametuhadithia Abdurrahman kutoka Zuhair kutoka Al-Alaa kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abu Hurairah kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wasallam, amesema: "Je, mnajua ni nani mfilisi?" Wakasema: Mfilisi kwetu, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni yule ambaye hana dirham wala bidhaa. Akasema: "Hakika mfilisi katika umma wangu ni yule anayekuja Siku ya Kiyama na funga, swala na zaka, na anakuja hali amemtukana heshima ya huyu, amemsingizia huyu, na amekula mali ya huyu, basi anakaa, na huyu analipwa kutokana na mema yake, na huyu kutokana na mema yake, na yakimalizika mema yake kabla ya kulipa madeni yake ya makosa, huchukuliwa kutoka katika makosa yao na kuwekwa juu yake, kisha anatupwa motoni."

Hakika hadithi hii, kama zilivyo hadithi zingine muhimu, ni lazima ieleweke maana yake na itambulike. Kwa sababu kuna watu ambao ni mafilisi licha ya swala zao, funga zao na zaka zao, kwani huyu alimtukana huyu, akamsingizia huyu, akala mali ya huyu, akamwaga damu ya huyu, na akampiga huyu  

Na ufilisi wake ni kwamba huchukuliwa kutoka kwa mema yake ambayo ni mtaji wake na hupewa huyu na hulipa kwa huyu thamani ya kumsingizia, kumtukana na kumpiga, na baada ya mema yake kwisha kabla ya kulipa madeni yake, huchukuliwa kutoka kwa makosa yao na kuwekwa juu yake kisha anatupwa motoni. 

Na alipowauliza Mtume, rehema na amani zimshukie, masahaba zake, je, mnajua ni nani mfilisi? Maana ya je, mnajua ni kutoka katika kujua na kujua ni elimu ya mambo ya ndani, je, mnajua, yaani mnajua nani hasa mfilisi? Hili linathibitisha kauli ya Sayyidina Ali, Mwenyezi Mungu aukurimishe uso wake: "Utajiri na umaskini ni baada ya kuonyeshwa kwa Mwenyezi Mungu." Walipoulizwa swali hili, walijibu jibu kutokana na uzoefu wao, mfilisi kwetu ni yule ambaye hana dirham wala bidhaa, huyu ndiye mfilisi kwa mtazamo wa masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi akasema, rehema na amani zimshukie: Hapana,... AKASEMA: HAKIKA MFILISI KATIKA UMMATI WANGU NI YULE ANAYEKUJA SIKU YA KIYAMA NA FUNGA, SWALA NA ZAKA... 

Na hili linathibitisha kauli ya Sayyidina Umar: Anayetaka afunge na anayetaka aswali lakini ni uadilifu, kwa sababu swala, funga, hijja na zaka hizi ni ibada ambazo mtu anaweza kuzifanya na katika nafsi yake kuna ikhlasi kwa ajili yake, na anaweza kuzifanya kwa unafiki, lakini kitovu cha uzito ni kujidhibiti kwa amri ya Mwenyezi Mungu 

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuthibitishe juu ya haki, na atufanye miongoni mwa waja wake wachaMungu, na atubadilishie maovu yetu kuwa mema, na asituhuzunishe siku ya kuonyeshwa Kwake, Ee Mwenyezi Mungu, Amina 

Wasikilizaji wetu wapendwa, na mpaka tukutane nanyi na hadithi nyingine ya Mtume, tunawaachia amana kwa Mwenyezi Mungu ambaye haipotezi amana zake, na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh 

Nimeiandika kwa ajili ya redio 

Afraa Turab

Pamoja na Hadithi Tukufu - Wanafiki na Matendo Yao Maovu

Pamoja na Hadithi Tukufu

Wanafiki na Matendo Yao Maovu

Tunawasalimu nyote wapenzi mahali popote mlipo, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imepokewa kutoka kwa Buraida Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ amesema: “Usimwite mnafiki bwana, kwa sababu ikiwa yeye ni bwana, basi mmemkasirisha Mola wenu Mlezi.” Imepokewa na Abu Daud kwa isnadi sahihi.

Enyi wasikilizaji wapenzi

Hakika maneno bora ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na uongofu bora ni uongofu wa Nabii wake Muhammad bin Abdullah, rehma na amani zimshukie, Ama baada ya hayo, 

Hakika hadithi hii tukufu inatuongoza jinsi ya kushughulika na wanafiki tunaowajua, kwani Mtume ﷺ alikuwa ndiye pekee anayewajua wanafiki wote kwa majina yao, lakini tunaweza kuwajua baadhi yao kutokana na sifa zao, kama wale ambao Qur'ani imewaelekeza kuwa wanafanya faradhi kwa uvivu na kwa kulazimishwa, na kama wale wanaowafanyia vitimbi Uislamu na Waislamu, wanahamasisha fitina, wanafanya uharibifu katika ardhi, wanapenda uovu uenee kwa kuualika, kuutetea na kuuchunga, na kama wale wanaosema uongo juu ya Uislamu na Waislamu ... na wengineo walio na sifa za unafiki. 

Kwa hivyo, lazima tutambue kile ambacho sheria imeona ni kizuri na kile ilichoona ni kibaya, ili tumjue mnafiki kutoka kwa mkweli, na tuchukue hatua inayofaa dhidi yake. Hatupaswi kuamini upande wa mtu ambaye anafanya kinyume na sheria na anaonekana kuwa anafanya anachokifanya kwa sababu ya bidii yake kwa Uislamu na Waislamu, na hatupaswi kumfuata au kumunga mkono, au hata chini ya hapo kwa kumuelezea kama bwana, vinginevyo Mwenyezi Mungu atatukasirikia.

Sisi Waislamu lazima tuwe watu wenye bidii zaidi kwa Uislamu na Waislamu, na tusimruhusu mnafiki yeyote kuingilia dini yetu na familia zetu, kwani wao ndio hatari zaidi tunayoweza kukumbana nayo siku hizi kwa sababu ya wingi wao na nyuso zao nyingi. Lazima tukumbuke mizani ya kisheria ya kupima matendo ya anayedai Uislamu, kwani Uislamu kwetu ni kinga dhidi ya watu hawa waovu. 

Tunamuomba Mungu aulinde umma wetu kutokana na wahalifu kama hao, na atuongoze kwenye njia iliyonyooka na mizani sahihi ambayo tunapima tabia za watu nayo, ili tujiepushe na wale ambao hawapendwi na Mungu, Aamin. 

Wapenzi wetu, na hadi tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya kinabii, tunawaacha katika uangalizi wa Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imeandikwa kwa ajili ya redio na: Dkt. Maher Saleh