Pamoja na Hadithi Tukufu
Kuahirisha Kulipa kwa Tajiri ni Dhuluma
3- Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji popote mlipo katika kipindi kipya cha programu yenu: PAMOJA NA HADITHI TUKUFU, tunaanza na salamu bora kabisa, Assalamu alaykum warahmatullah wabarakatuh
Ibn Maajah, Allah amrehemu, ameipokea kwamba Mtume ﷺ amesema: "Kuahirisha kulipa deni kwa tajiri ni dhuluma, na mnapo pewa uhakika wa kulipwa na mwenye uwezo, basi mfuateni", na pia amepokea, Allah amrehemu, kutoka kwa Mtume ﷺ kwamba yeye alisema: "Ukaidi wa mwenye nacho hu halalalisha heshima yake na adhabu yake."
Na wanavyuoni wamesema kuhusu kauli yake ﷺ: "Ukaidi wa mwenye nacho huhalalisha heshima yake," kwa kusema (amenichelewesha), na adhabu yake ni kufungwa mpaka amlipe.
Ibn Abbas, Allah amridhie, amesema: [Ameruhusiwa kumuomba Allah amlaani aliyemdhulumu, na namna ya kuomba ni kusema: Ee Allah nisaidie juu yake, Ee Allah nitoe haki yangu kwake, Ee Allah tenganisha baina yangu na yeye].
Na maimamu wamepokea kutoka kwa Aisha, Allah amridhie, kwamba yeye alimsikia mtu akimuomba Allah amlaani mwizi aliyemuibia, akasema: [Usimwonee haya] yaani usipunguze maombi yako, na hii ni ikiwa ni muumini, lakini ikiwa ni kafiri basi achia ulimi wako na uombe maangamizi.
Wasikilizaji wetu wapenzi:
Hakika watawala wa zama hizi wote wametucheleweshea haki zetu, ni nani atawafunga? Hakika wametudhulumu, ni nani atatulipia kisasi kutoka kwao? Hakika wametuibia, ni nani atawaadhibu? Hakika kuwafunga watawala na kulipiza kisasi kutoka kwao na kuwaadhibu hakutakuwa isipokuwa na dola ya Khilafa ijayo InshaAllah, ambayo itatekeleza juu yao hukumu ya Allah ambayo itaponya vifua vya umma, na kwa kila anayetaka kuadhibu watawala kwa uhalifu wao na maovu yao, basi ajiunge na msafara wa heri ambao unataka kuwabadilisha na kuondoa mizizi yao ili kusimamisha hukumu ya Allah kupitia dola ya Khilafa, kisha tufanye pamoja na kazi ngumu ya kuwabadilisha kulingana na hukumu za sheria tunachotaka cha kuwaombea mabaya kama vile kusema: Ee Allah wahesabu kwa idadi na uwaue kwa vipande vipande wala usiache hata mmoja wao, Ee Allah usidumishe utawala wao wala usiwainue bendera na uwafanye kuwa mazingatio na ishara kwa watu, Ee Allah tufanye tuwaharakishe kwako kwani Wewe ni Mlipiza kisasi Mwenye nguvu.
Wasikilizaji wetu wapenzi
Na mpaka tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya Nabii, tunawaacha katika ulinzi wa Allah, na Assalamu alaykum warahmatullah wabarakatuh