Ma Hadithi Tukufu
Urithi wa Manabii
Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji popote mlipo katika kipindi kipya cha programu yenu: Ma Hadithi Tukufu, na tunaanza na salamu bora kabisa, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Dardaa kwamba alisema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema: "Yeyote anayefuata njia ya kutafuta elimu, Mwenyezi Mungu atamfuatilisha njia ya kwenda Peponi. Na hakika Malaika huweka mabawa yao kwa kumridhia mwanafunzi wa elimu. Na hakika kila aliye katika mbingu na ardhi humwombea msamaha mwanachuoni, hata samaki waliomo ndani ya maji. Na ubora wa mwanachuoni juu ya mcha Mungu ni kama ubora wa mwezi juu ya sayari zote. Hakika wanachuoni ni warithi wa Manabii. Hawakuacha urithi wa dinari wala dirham, bali waliacha urithi wa elimu. Basi yeyote atakayeichukua, amechukua fungu kubwa." Imepokewa na Ahmad katika Musnad yake kwa mabadiliko kidogo.
Imaam Ahmad, Allah amrehemu, amesema: [Hawa ndio watawala wa mambo baada yake, nao ni maamiri na wanachuoni].
Wasikilizaji wetu wapenzi
Hakika watawala wa zama hizi wameharibika wote, hakuna hata mmoja wao anayesimamisha sheria wala kusikiliza amri yake wala makatazo yake, wote wamegeuza migongo yao kwa wito wa haki na kuinusuru, bali wamekubaliana kupigana nayo na kuwazuia watu wake, kwa hivyo hakuna kheri dhahiri kwao inayotarajiwa, bali kila kilicho ndani yao ni shari, hila na udanganyifu, wamejitoa wenyewe kutoka kwa warithi wa Muhammad ﷺ, na hawakubaki warithi wake isipokuwa Waislamu na wafanyakazi wa kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu ardhini ambao wamejitenga na watawala waziwazi na wanaongoza umma kuelekea kufanya kazi ya kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu. Na majeshi ambayo yanawakilisha vituo vya nguvu na wao ndio wana uwezo wa kuwaondoa watawala kwa ajili ya kumsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kusaidia dini yake, na umma, haya ndiyo yaliyosalia kutoka kwa warithi wa Bwana wetu Muhammad ﷺ, kwa hivyo kila mrithi achukue sehemu yake kutoka kwa urithi na atekeleze haki yake na anayostahiki mpaka kisimame dola la Khilafa, dola la Qur'ani na Sunna ambalo wakati wake umefika, basi Ee Mwenyezi Mungu tufanye miongoni mwa askari wake na mashahidi wake.
Wasikilizaji wetu wapenzi
Na hadi tutakapokutana na hadithi nyingine ya kinabii tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh