Ma Hadithi - Lau Mngelikuwa Kama Mnavyokuwa Nami
Ma Hadithi - Lau Mngelikuwa Kama Mnavyokuwa Nami

 Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali katika kipindi kipya cha programu yenu Ma Hadithi Tukufu na tunaanza na salamu bora kabisa, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

0:00 0:00
Speed:
July 22, 2025

Ma Hadithi - Lau Mngelikuwa Kama Mnavyokuwa Nami

 Ma Hadithi - Lau Mngelikuwa Kama Mnavyokuwa Nami

 Tunawasalimu nyote wapenzi wasikilizaji kila mahali katika kipindi kipya cha programu yenu Ma Hadithi Tukufu na tunaanza na salamu bora kabisa, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh ,

KUTOKA KWA HANTHALA AL-KATIBU AT-TAMIMI AL-USAYYIDI AMESEMA:

"Tulikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimshukie, tukitaja pepo na moto hata kama vile tunaziona kwa macho, nikaondoka kwa familia yangu na watoto wangu nikacheka na kucheza, akasema: Nikakumbuka tuliyokuwa nayo, nikatoka nikakutana na Abu Bakr nikasema: Nimemfanyia unafiki, nimemfanyia unafiki, Abu Bakr akasema: Hakika tunafanya hivyo, Hanthala akaenda akamtajia Mtume, rehema na amani zimshukie akasema: Ewe Hanthala lau mngelikuwa kama mnavyokuwa kwangu bila shaka Malaika wangewasalimu kwenye matandiko yenu au kwenye njia zenu, ewe Hanthala saa na saa"

Imekuja katika ufafanuzi wa Sunan Ibn Majah ya As-Sindi

Kauli yake (Nimefanya unafiki) yaani hali yangu imebadilika kwa namna ambayo haifai kughafilika nazo kwa anayeziamini, basi kughafilika nazo kunafanana na kuwa ni katika kukataa kwa ndani uwepo wake na kwa jumla basi ameshawishika juu ya kuwepo kwa imani nazo katika moyo wake bila shaka na amehesabu kuwa ni unafiki na kwa hili imedhihirika kuwa shaka katika imani si yenye kukufurisha bali shaka katika anayeaminiwa ndio yenye kukufurisha.

Kauli yake (Lau mngelikuwa kama mnavyokuwa)

Amewakumbusha kuwa kuhudhuria hakudumu kikawaida na kutokuhudhuria hakudhuru katika kuwepo imani moyoni na kughafilika kunapingana na kuhudhuria basi hailazimu kutoka kwake kutokuwepo imani; saa inakuwa kuhudhuria ili mambo ya dini yatengemae kwayo na saa inakuwa kughafilika ili mambo ya dini na maisha yatengemae kwayo na katika kila moja katika hayo kuna rehema kwa waja.

Wasikilizaji wetu wapenzi:

Hadithi Tukufu ambayo mikononi mwetu inathibitisha mambo kadhaa, miongoni mwao:

Kwanza: Dhana ya (saa na saa) haina uhusiano wowote nayo, si karibu wala mbali na anavyoelewa baadhi ya watu kuwa saa ni yako na saa ni ya Mola wako. Kwani imekwisha bainika kuwa maisha ya Muislamu yote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu akiwafundisha waja wake waseme (Sema hakika sala yangu na ibada zangu na uhai wangu na umauti wangu ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu)

Basi hakuna katika maisha ya Muislamu chochote kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu (Amenunua kutoka kwa waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao wana pepo) basi Waislamu wote wameuza wanachokimiliki kuwa thamani ya pepo, naam inaweza kuwepo katika maisha ya Muislamu saa ya kuamka na saa ya kughafilika, na saa ya nguvu na saa ya udhaifu, na saa ya ukaribu na saa ya umbali, lakini haraka anazinduka na kuona; basi anaondoa kughafilika na anaongeza nguvu udhaifu, na anakimbilia kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Amesema: (Hakika wale ambao wamemcha Mungu pindi wanapoguswa na wasiwasi kutoka kwa shetani hukumbuka ndipo wao huona)

Na imekuja katika Hadithi Tukufu: (Kila mwanaadamu anakosea na mbora wa wakoseaji ni wenye kutubu)

Pili: Kwamba mawaidha na uongozi haitoshi peke yake ili iwe njia katika kujenga haiba na kubadilisha tabia. Basi pepo na moto na kuogopesha na kutamanisha vyote ni katika Uislamu. Lakini inapaswa wasighafilike wanazuoni wetu na wabebaji wa daawa kuwa hakuna budi pia na fikra na dhana za Kiislamu ambazo anazihitajia kila Muislamu katika maisha yake ya kila siku ambazo zinaathiri tabia yake athari yenye kuleta matokeo na iliyo na umakini. Basi kwa Muislamu pamoja na ufahamu wake wa neema za pepo na adhabu za akhera, anatakiwa afahamu kwa mfano ukweli wa mapambano kati ya Uislamu na ukafiri na afahamu ukweli wa demokrasia na ulaikini na ubepari na afahamu ukweli wa itikadi za Kiislamu kwa kuwa ni itikadi ya kiroho na kisiasa na afahamu kuwa Uislamu umekuja utekelezwe na afahamu kuwa hakuna utekelezaji wa Uislamu ila kwa dola na afahamu sababu za kuchelewa kwetu na njia ya kuinuka kwetu.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: 

(Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na wale walio pamoja naye ni wakali kwa makafiri wenye huruma baina yao unawaona wanarukuu wanasujudu wanatafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi alama zao ziko katika nyuso zao kutokana na athari za kusujudu hiyo ni mfano wao katika Taurati na mfano wao katika Injili kama mmea uliochipua tawi lake kisha ukautia nguvu kisha ukawa mnene kisha ukasimama sawa juu ya shina lake unawapendeza wakulima ili awakasirishe makafiri kwao Mwenyezi Mungu Amewaahidi wale ambao wameamini na wametenda mema miongoni mwao msamaha na ujira mkubwa)

Na Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Kueni wachaMungu kwa sababu ya kuwa mlikuwa mnafundisha kitabu na kwa sababu ya kuwa mlikuwa mnasoma)

Wasikilizaji wetu wapenzi na mpaka pale tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya kinabii tunawaacha katika hifadhi ya Mwenyezi Mungu na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

More from Sheria

Pamoja na Hadithi Tukufu - Je, mnajua ni nani mfilisi?

Pamoja na Hadithi Tukufu

Je, mnajua ni nani mfilisi?

Karibuni wasikilizaji wetu wapendwa, wasikilizaji wa redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir. Tunakutana nanyi tena na kipindi chetu pamoja na Hadithi Tukufu, na bora tuanzie nayo kipindi chetu ni salamu ya Kiislamu, basi Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imekuja katika Musnad Ahmad - sehemu iliyobaki ya Musnad ya Al-Mukthirin - Hakika mfilisi katika umma wangu ni yule anayekuja Siku ya Kiyama na funga na swala na zaka, na anakuja hali amemtukana huyu, amemsingizia huyu, na amekula mali ya huyu 

  Ametuhadithia Abdurrahman kutoka Zuhair kutoka Al-Alaa kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abu Hurairah kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wasallam, amesema: "Je, mnajua ni nani mfilisi?" Wakasema: Mfilisi kwetu, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni yule ambaye hana dirham wala bidhaa. Akasema: "Hakika mfilisi katika umma wangu ni yule anayekuja Siku ya Kiyama na funga, swala na zaka, na anakuja hali amemtukana heshima ya huyu, amemsingizia huyu, na amekula mali ya huyu, basi anakaa, na huyu analipwa kutokana na mema yake, na huyu kutokana na mema yake, na yakimalizika mema yake kabla ya kulipa madeni yake ya makosa, huchukuliwa kutoka katika makosa yao na kuwekwa juu yake, kisha anatupwa motoni."

Hakika hadithi hii, kama zilivyo hadithi zingine muhimu, ni lazima ieleweke maana yake na itambulike. Kwa sababu kuna watu ambao ni mafilisi licha ya swala zao, funga zao na zaka zao, kwani huyu alimtukana huyu, akamsingizia huyu, akala mali ya huyu, akamwaga damu ya huyu, na akampiga huyu  

Na ufilisi wake ni kwamba huchukuliwa kutoka kwa mema yake ambayo ni mtaji wake na hupewa huyu na hulipa kwa huyu thamani ya kumsingizia, kumtukana na kumpiga, na baada ya mema yake kwisha kabla ya kulipa madeni yake, huchukuliwa kutoka kwa makosa yao na kuwekwa juu yake kisha anatupwa motoni. 

Na alipowauliza Mtume, rehema na amani zimshukie, masahaba zake, je, mnajua ni nani mfilisi? Maana ya je, mnajua ni kutoka katika kujua na kujua ni elimu ya mambo ya ndani, je, mnajua, yaani mnajua nani hasa mfilisi? Hili linathibitisha kauli ya Sayyidina Ali, Mwenyezi Mungu aukurimishe uso wake: "Utajiri na umaskini ni baada ya kuonyeshwa kwa Mwenyezi Mungu." Walipoulizwa swali hili, walijibu jibu kutokana na uzoefu wao, mfilisi kwetu ni yule ambaye hana dirham wala bidhaa, huyu ndiye mfilisi kwa mtazamo wa masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi akasema, rehema na amani zimshukie: Hapana,... AKASEMA: HAKIKA MFILISI KATIKA UMMATI WANGU NI YULE ANAYEKUJA SIKU YA KIYAMA NA FUNGA, SWALA NA ZAKA... 

Na hili linathibitisha kauli ya Sayyidina Umar: Anayetaka afunge na anayetaka aswali lakini ni uadilifu, kwa sababu swala, funga, hijja na zaka hizi ni ibada ambazo mtu anaweza kuzifanya na katika nafsi yake kuna ikhlasi kwa ajili yake, na anaweza kuzifanya kwa unafiki, lakini kitovu cha uzito ni kujidhibiti kwa amri ya Mwenyezi Mungu 

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuthibitishe juu ya haki, na atufanye miongoni mwa waja wake wachaMungu, na atubadilishie maovu yetu kuwa mema, na asituhuzunishe siku ya kuonyeshwa Kwake, Ee Mwenyezi Mungu, Amina 

Wasikilizaji wetu wapendwa, na mpaka tukutane nanyi na hadithi nyingine ya Mtume, tunawaachia amana kwa Mwenyezi Mungu ambaye haipotezi amana zake, na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh 

Nimeiandika kwa ajili ya redio 

Afraa Turab

Pamoja na Hadithi Tukufu - Wanafiki na Matendo Yao Maovu

Pamoja na Hadithi Tukufu

Wanafiki na Matendo Yao Maovu

Tunawasalimu nyote wapenzi mahali popote mlipo, katika kipindi kipya cha programu yenu "Pamoja na Hadithi Tukufu" na tunaanza na salamu bora, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imepokewa kutoka kwa Buraida Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ amesema: “Usimwite mnafiki bwana, kwa sababu ikiwa yeye ni bwana, basi mmemkasirisha Mola wenu Mlezi.” Imepokewa na Abu Daud kwa isnadi sahihi.

Enyi wasikilizaji wapenzi

Hakika maneno bora ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na uongofu bora ni uongofu wa Nabii wake Muhammad bin Abdullah, rehma na amani zimshukie, Ama baada ya hayo, 

Hakika hadithi hii tukufu inatuongoza jinsi ya kushughulika na wanafiki tunaowajua, kwani Mtume ﷺ alikuwa ndiye pekee anayewajua wanafiki wote kwa majina yao, lakini tunaweza kuwajua baadhi yao kutokana na sifa zao, kama wale ambao Qur'ani imewaelekeza kuwa wanafanya faradhi kwa uvivu na kwa kulazimishwa, na kama wale wanaowafanyia vitimbi Uislamu na Waislamu, wanahamasisha fitina, wanafanya uharibifu katika ardhi, wanapenda uovu uenee kwa kuualika, kuutetea na kuuchunga, na kama wale wanaosema uongo juu ya Uislamu na Waislamu ... na wengineo walio na sifa za unafiki. 

Kwa hivyo, lazima tutambue kile ambacho sheria imeona ni kizuri na kile ilichoona ni kibaya, ili tumjue mnafiki kutoka kwa mkweli, na tuchukue hatua inayofaa dhidi yake. Hatupaswi kuamini upande wa mtu ambaye anafanya kinyume na sheria na anaonekana kuwa anafanya anachokifanya kwa sababu ya bidii yake kwa Uislamu na Waislamu, na hatupaswi kumfuata au kumunga mkono, au hata chini ya hapo kwa kumuelezea kama bwana, vinginevyo Mwenyezi Mungu atatukasirikia.

Sisi Waislamu lazima tuwe watu wenye bidii zaidi kwa Uislamu na Waislamu, na tusimruhusu mnafiki yeyote kuingilia dini yetu na familia zetu, kwani wao ndio hatari zaidi tunayoweza kukumbana nayo siku hizi kwa sababu ya wingi wao na nyuso zao nyingi. Lazima tukumbuke mizani ya kisheria ya kupima matendo ya anayedai Uislamu, kwani Uislamu kwetu ni kinga dhidi ya watu hawa waovu. 

Tunamuomba Mungu aulinde umma wetu kutokana na wahalifu kama hao, na atuongoze kwenye njia iliyonyooka na mizani sahihi ambayo tunapima tabia za watu nayo, ili tujiepushe na wale ambao hawapendwi na Mungu, Aamin. 

Wapenzi wetu, na hadi tutakapokutana nanyi na hadithi nyingine ya kinabii, tunawaacha katika uangalizi wa Mungu, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Imeandikwa kwa ajili ya redio na: Dkt. Maher Saleh