Muda mfumo wa kilimwengu ukiwa bado upo, mashambulizi dhidi ya maadili yetu hayataacha!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Jarida la kila wiki la Leman lilichapisha katuni ya kukera katika toleo lake la Juni 26, 2025. Katuni hiyo inamuonyesha Nabii Muhammad ﷺ akisema: "Asalamu Alaikum, mimi ni Muhammad," na Nabii Musa akamjibu: "Alaikum Salam, mimi ni Musa," dhidi ya mzozo. Ghadhabu ya umma ilisababisha ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu huko Istanbul kufungua uchunguzi na kutoa agizo la kukamata mchoro huo. (Mashirika ya habari, Juni 30, 2025)
Maoni:
Jarida la Leman limevuka mipaka yake kwa kumuonyesha Nabii Muhammad ﷺ, ambaye Waislamu hawamtaji ila kwa kumtakia sala na salamu, na Nabii Musa, amani iwe juu yake, katika katuni mbaya.
Na kwa kuenea kwa mada hiyo kwenye mitandao ya kijamii, Waislamu walimiminika katika Mtaa wa Istiklal huko Taksim kufanya maandamano kwa hasira. Wizara ya Mambo ya Ndani iliingilia kati na kuwakamata waliohusika na katuni hiyo. Picha za maadui hao wa Uislamu, wakiwa wamefungwa pingu na wakikokotwa hadi kituo cha polisi bila viatu, zilipunguza mvutano kati ya Waislamu.
Erdogan na wanasiasa wengine walibadilishana ujumbe unaoonyesha upendo wao kwa Nabii ﷺ. Serikali ilituliza hasira ya maoni ya umma kwa matamshi ya kutuliza. Maafisa walikamatwa na kufungwa. Lakini hakuna kingine kilichotokea, kwa sababu mfumo wa sasa wa kisheria, ambao umeondoa mawazo ya Nabii kutoka kwa maisha ya umma, hauruhusu hatua nyingine yoyote.
Katika mfumo huu, sheria zinamkinga Mustafa Kemal na rais dhidi ya matusi, lakini hakuna sheria maalum ya kumlinda Muhammad ﷺ, ambaye ndiye thamani kuu na mwongozo kwa Waislamu. Hili halishangazi, kwani sheria zinaakisi itikadi ya taifa iliyochaguliwa. Katika mifumo ya kilimwengu ambayo inazingatia upinzani dhidi ya Mungu na Mtume Wake ﷺ kama itikadi rasmi, dini inakuwa tu suala la dhamiri binafsi, iliyozuiliwa kuathiri maisha ya umma. Wito wa ushawishi wa kidini, au kuunda chama cha siasa kwa ajili yake, ni uhalifu chini ya sheria ya Kituruki. Kwa hivyo matamshi ya serikali yanayomtetea Nabii ﷺ ni ishara tu za kihemko ambazo hazina msingi wowote wa kweli ﴿Je! Hukuwaona wale wanadai kuwa wameamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka kwenda kuhukumiwa kwa taghuti, nao wameamrishwa kumkataa?﴾.
Mara nyingi matamshi kama haya ya kisiasa yanalenga kutumia hisia za Waislamu. Mfano wa wazi wa hii ni ushiriki wa Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu katika mazishi ya Paris baada ya shambulio la Charlie Hebdo mnamo 2015, tukio ambalo limezikwa katika kumbukumbu za Waislamu kama alama ya aibu.
Kwa hivyo, madai ya viongozi wanaojiita wahafidhina wa kidemokrasia juu ya upendo wao kwa Nabii, Uislamu na kuutetea ni faraja tu. Uaminifu wao wa kweli uko katika misimamo yao, washirika wao wa Magharibi, na mfumo wa kilimwengu wa asili ya Magharibi. Ukweli huu unathibitishwa na matukio mengi ya uchungu, usaliti, na ushawishi mbaya wa demokrasia.
Kuondoa Sunnah za Nabii ﷺ kutoka kwa maisha, na kuacha Msikiti wa Al-Aqsa, Gaza, na ardhi takatifu ya Isra na Mi'raj kwa uvamizi wa Kisalaba wa Kizayuni na mauaji wanayoyafanya, ni moja ya matusi makubwa kwa Nabii ﷺ na maadili yetu.
Ama walimwengu, Wakemali, Wakomunisti, makafiri, na wengineo wenye kanuni za kupinga Uislamu wanaotetea michoro kama hii, hatima yao ni kushindwa na Jahannamu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtuma Muhammad ﷺ kama rehema, akakiinua cheo chake, na akawadhalilisha washambuliaji wake katika dunia hii na Akhera. Na sheria hii ya Kiungu haibadiliki kamwe.
Na kila Muislamu anayempenda Mwenyezi Mungu, Mtume wake, na waumini lazima afanye kazi ya kuanzisha dola ya Khilafah, ambayo inalinda Uislamu, kuutekeleza, na kuueneza kama mwongozo kwa watu wote. La sivyo, mradi tu mfumo wa kilimwengu unabaki umeunganishwa na ukafiri wa kimataifa, mashambulizi dhidi ya maadili yetu yataendelea. «Hatamini mmoja wenu mpaka mimi niwe mpendwa zaidi kwake kuliko mzazi wake, mtoto wake, na watu wote». (Sahih Bukhari)
Imeandikwa kwa Redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Muhammad Amin Yildirim