Upofu huu unaofunika busara huko Iran ni nini?!
Habari:
Waziri wa mambo ya nje wa Iran anaitaka Umoja wa Mataifa kuubebesha utawala wa Kiyahudi na Marekani jukumu la shambulio dhidi yake na anataka fidia, na Iraqchi alielekeza ujumbe kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambapo aliitaka Baraza la Usalama "kuutambua utawala wa Israel na Marekani kama waanzilishi wa uchokozi, na kuubebesha jukumu kamili kwa hilo, ikiwa ni pamoja na kulipa fidia na kulipia uharibifu uliosababishwa". (RT, 29/6/2025)
Maoni:
Ikiwa viongozi wa Iran kupitia ujumbe huu kwa Umoja wa Mataifa, ambao wanajua kuwa Marekani inaudhibiti kikamilifu, wanautaka kulaani Marekani na utawala wa Kiyahudi kwa sababu ya kuanzisha uchokozi dhidi ya Iran, yaani, wanaitaka Marekani kujilaani yenyewe, ikiwa wanafikiri kuwa hili linawezekana, basi huu ndio upofu usio na mwisho, na hatufikirii wako hivyo.
Na ikiwa wanafikiri kwamba wako mbele ya watu wao wanafanya kitendo baada ya shambulio kali ambalo Iran ilifanyiwa na kusababisha vifo vya idadi ya viongozi wao wakuu na wasomi na sehemu kubwa ya mpango wao wa nyuklia, basi huu ni upotoshaji wa kisiasa, na ikiwa upotoshaji wa kisiasa unalenga watu, basi unaitwa usaliti, yaani, ni mkubwa kuliko upotoshaji.
Iran ingeweza kujitetea vyema zaidi! Ripoti zote zilikuwa zikizungumzia kuhusu kumalizika kwa akiba ya utawala wa Kiyahudi wa risasi za ulinzi wa anga, yaani, utawala wa Kiyahudi ulikuwa unakabiliwa na kufichuliwa anga zake kwa makombora ya Iran kama vile anga za Iran zilivyokuwa wazi kwa ndege zake, ndege hizo ambazo Marekani iliipa sababu zote za kufaulu, kama vile kupita karibu na kambi zake za kijeshi nchini Syria, Iraq na Jordan na kuzipatia mafuta na kushirikisha habari za kijasusi, hivyo Iran ingeweza kusubiri na kutokubali kusitisha mapigano hasa ikizingatiwa kuwa utawala wa Kiyahudi una hisia kali kwa hasara, lakini haukufanya hivyo!
Iran ingeweza kuzishambulia kambi za kijeshi za Marekani katika Ghuba, kabla ya Marekani kutoa vifaa na wanajeshi kutoka humo na ilikuwa inajiandaa kushiriki hadharani katika vita, lakini haikufanya hivyo. Na Iran ingeweza kushirikisha vikosi vyake vya ardhini na kushambulia Iraq na kuipindua serikali vibaraka ya Marekani na kuzishambulia maslahi ya Marekani na kukaribia utawala wa Kiyahudi, na makombora yake ya masafa mafupi yangeweza kuufikia, na hata ingeweza kushirikisha vikosi vyake vya majini na kuzipindua tawala katika Falme za Kiarabu, Bahrain na Qatar ambazo zinashirikiana na Marekani na kutekeleza sera zake na kuziteka kambi za kijeshi za Marekani humo, na kuipindua meza dhidi ya Marekani kwa kupanua vita, na kuipindua meza dhidi ya Magharibi yote kwa kuizuia mafuta na kuvuruga gurudumu lake la kiuchumi mpaka Marekani na Ulaya pamoja nayo zipige kelele kwamba simamisheni vita.
Na lau Iran ingefanya mojawapo ya harakati hizi kubwa, ingeweza kuweka masharti na kudai kuibebesha Marekani na utawala wa Kiyahudi jukumu, lakini haikufanya chochote kati ya hayo na ilitosheka tu na kwamba kichwa cha utawala kimeokoka!
Na leo wanadai kubeba jukumu na fidia, na la kushangaza zaidi ni kwamba wanafanya mazungumzo na Marekani nyuma ya pazia, bali bila pazia! Vipi ushindi utakuwa mshirika wenu na hamthubutu kufanya matendo kama hayo na mnamngojea adui yenu afungue mazungumzo nanyi?!
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya afisi ya habari kuu ya Hizb ut Tahrir
Bilal Al-Tamimi