Inaungwa mkono na Magharibi, na inalindwa na majirani zake
(Imetafsiriwa)
Habari:
Netanyahu anaongeza msimamo wake kuhusu usalama wa taasisi yake kabla ya kukutana na Vance. (Associated Press)
Maoni:
Katika mkutano wake wa hivi majuzi na Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance, Benjamin Netanyahu alitangaza kwamba nchi yake haijalindwa na Marekani, akidai uhuru wake kamili katika maamuzi yake ya kiusalama na kisiasa. Ameionyesha kama nguvu huru, iliyo mbali na ushawishi wa Washington. Hata hivyo, tangazo hili lilikuja wakati ambapo Marekani inaendelea kulazimisha mdundo wake wa kisiasa katika mazungumzo na mipango ya kusimamisha vita dhidi ya Gaza.
Madai haya ya uhuru ni jaribio la wazi la kuonyesha nguvu wakati ambapo uhalali na utulivu wa taasisi ya Kiyahudi unategemea kabisa ngao ya msaada wa Magharibi. Kwa kweli, taasisi hii si kitu ila kituo cha mbele cha operesheni za kijeshi, kiintelijensia na kisiasa za mfumo wa kikoloni wa Magharibi uliopandwa katika moyo wa nchi za Kiislamu. Uwepo na uhai wake unategemea mtiririko endelevu wa misaada ya kijeshi ya Marekani, kubadilishana habari za kiintelijensia na msaada wa kiuchumi wa mabilioni ya dola kila mwaka; kutoka kwa mfumo wa Iron Dome hadi vikosi vyake vya anga vinavyotegemea ndege za Marekani, na uchumi unaoungwa mkono na biashara ya Magharibi, uwekezaji na fedha za walipa kodi wa Marekani. Kila mshipa muhimu wa uhai wa taasisi hii unaungwa mkono kutoka nje. Bila msaada huu, haiwezi kustahimili hata siku moja ya mapambano ya kijeshi yanayoendelea.
Hotuba ya Netanyahu ni jaribio la kukata tamaa la kudumisha udanganyifu wa nguvu na uhuru huku ulimwengu ukishuhudia ukweli: taasisi ya Kiyahudi ipo tu kama pando la kikoloni linalohudumia maslahi ya kimkakati ya Magharibi kugawanya nchi za Kiislamu na kuzuia umoja wake wa kisiasa na kudumisha udhibiti wa Magharibi juu ya rasilimali za eneo hilo na mwelekeo wake wa kisiasa. Kuendelea kuishi kwake pia kunahakikishwa na serikali zinazoizunguka huko Jordan, Misri na Uturuki, ambazo hufanya kazi kama walinzi wa kikanda. Pamoja, serikali hizi huunda pete ya ulinzi ambayo inalinda mradi wa Kizayuni kutokana na makabiliano ya kweli, na kuuiweka kama kituo cha Magharibi kilichoanzishwa katika moyo wa nchi za Kiislamu.
Ukweli usiopingika ni kwamba taasisi ya Kiyahudi haipo ila kwa sababu ya ulinzi wa Magharibi na usaliti wa serikali zinazoizunguka. Kuondoa safu moja ya usalama huu bandia kutamaliza mradi mzima. Haibaki kwa nguvu yake ya asili, lakini kwa unyenyekevu wa wale wanaoisaidia. Ni pale tu umma wa Kiislamu utakapogundua ukweli huu na kurejesha Ukhalifa kwa njia ya Unabii ndipo eneo hilo litarudi katika hali yake ya kawaida, likiwa huru kutoka kwa kituo hiki cha kikoloni na serikali zinazolinda.
Imeandikwa kwa idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Haitham bin Thabit
Mwakilishi wa Habari wa Hizb ut-Tahrir huko Amerika