Nani Atawaokoa Waislamu wa Rohingya Kutokana na Ghasia, Dhuluma na Mauaji?
Habari:
Ripoti mpya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyochapishwa hivi karibuni ilisema kuwa jeshi la Myanmar liliharibu kabisa vijiji na misikiti ya Rohingya ili kujenga vituo vya usalama, na ilisema: Ghasia dhidi ya Rohingya ziliongezeka sana mnamo Agosti 2017 wakati jeshi la Myanmar lilipoanzisha operesheni ya kijeshi kujibu mashambulizi ya wanamgambo, ambayo ilisababisha mamia ya maelfu ya watu kuyahama makazi yao katika jimbo la pwani.
Takriban wakimbizi milioni 1.3 wa Rohingya sasa wanaishi katika kambi zilizojaa watu nchini Bangladesh, kufuatia operesheni ya kijeshi ambayo Umoja wa Mataifa baadaye uliielezea kama "mfano wazi wa utakaso wa kikabila" na kubadilisha ardhi yao kuwa vituo vya usalama.
Ripoti hiyo ilitolewa siku moja kabla ya mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa huko New York ambao unalenga mzozo wa Rohingya, ambapo maafisa watajadili kuzorota kwa hali katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh na juhudi za kuwarejesha makwao zinakwama.
Kwa mfano, katika eneo la kijiji cha Inn Din, ambapo Reuters iliripoti mwaka 2018 juu ya kuuawa kwa wanaume 10 wa Rohingya, jeshi liliharibu makazi ili kujenga kituo kipya, kulingana na utaratibu huru wa uchunguzi nchini Myanmar.
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa kambi hiyo "ilijengwa moja kwa moja juu ya magofu ya vijiji vya Inn Din (mashariki mwa Rakhine), na ardhi iliyosafishwa ikibadilishwa na barabara mpya, majengo ya kudumu, majengo ya makazi yaliyoimarishwa na helikopta mbili."
Maoni:
Mashirika hayo kama vile Umoja wa Mataifa au utaratibu huru wa uchunguzi nchini Myanmar hayajatatua na hayatatatua kamwe matatizo ya Waislamu. Wanajionyesha kana kwamba wanajali na wanashughulika na matatizo ya wakimbizi, wanaandaa mabaraza, wanakutana, wanajadili kuhamisha wakimbizi kwenda nchi zao, na wanatuma wafanyakazi wao kuona kwa macho yao kile kinachotokea katika kambi za wakimbizi, lakini ulimwengu mzima unashuhudia kile kinachotokea katika maeneo ya Waislamu kutokana na ghasia, dhuluma na mauaji, na kutokana na majanga ambayo Waislamu wanakabiliwa nayo ya njaa na magonjwa, na uhaba wa mahitaji muhimu ya maisha, licha ya ukweli kwamba nchi zao zimejaa rasilimali za asili ambazo Mungu Mtukufu amewapa. Haya yote ni mchezo, uwongo, usaliti na jukwaa ambalo waigizaji hufanya majukumu yao kwa ustadi na ukamilifu.
Enyi Waislamu: Msitamani wala msingojee msaada wa kujiokoa wenyewe na mali zenu, kwa sababu makafiri na wakoloni ndio adui, na Mungu Mtukufu ametujulisha wao katika Kitabu chake Kitukufu: ﴿Hakika utawakuta walio na uadui mkali zaidi kwa walio amini ni Mayahudi na wale walio shiriki﴾.
Matatizo hayo yataisha lini, na ni nani atawarejesha wakimbizi kwenye nyumba zao, na atawazuia makafiri kufanya dhuluma na ghasia dhidi ya Waislamu kote ulimwenguni? Na Waislamu wataweza kuishi katika nyumba zao lini bila hatari katika usalama na utulivu?
Chini ya mfumo wa Kiislamu, raia na nyumba zinalindwa dhidi ya uharibifu, wenye njaa wanalishwa na wanatolewa mahitaji ya msingi ambayo wanahitaji ili kufurahia maisha mazuri.
Kwa hivyo, kusubiri msaada kutoka kwa mashirika na taasisi zinazofadhiliwa na makafiri ambao ndio sababu ya kurudi nyuma kwa Waislamu katika nyanja zote sio sahihi. Kuwaokoa Waislamu kutoka kwa migogoro ya kiuchumi na kisiasa kunawatisha makafiri, kwa sababu wanajua vizuri kwamba Waislamu wakiamka, watarudi kwenye utukufu wao, heshima yao na nguvu zao ambazo walipoteza baada ya kubomolewa kwa Dola ya Kiislamu, na hivyo makafiri watapoteza utajiri, nafasi na uongozi.
Tunapaswa kutibu chanzo cha ugonjwa badala ya kuondoa dalili, na hapo ndipo dhuluma na matatizo yataisha na kusimama kote ulimwenguni, na watoto wanajifunza shuleni, na mama hawahisi wasiwasi juu ya watoto wao, na wazee na wanawake wanaishi kwa utulivu.
Siku hizo ziko karibu sana, kwa sababu ulimwengu unaishi chini ya mfumo dhalimu, na baada yake itakuja Ukhalifa ulioongoka ambao Mungu Mtukufu aliahidi na Mtume ﷺ alitabiri kurudi kwake katika yale ambayo Imamu Ahmad alisimulia katika Musnad kutoka kwa Hudhaifa, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: «Utume utakuwa miongoni mwenu kwa muda ambao Mungu atapenda uwe, kisha atauondoa atakapopenda kuuondoa, kisha kutakuwa na ukhalifa juu ya njia ya utume, utakuwa kwa muda ambao Mungu atapenda uwe, kisha atauondoa atakapopenda kuuondoa, kisha kutakuwa na ufalme wa kuuma, utakuwa kwa muda ambao Mungu atapenda uwe, kisha atauondoa atakapopenda kuuondoa, kisha kutakuwa na ufalme wa kidhalimu, utakuwa kwa muda ambao Mungu atapenda uwe, kisha atauondoa atakapopenda kuuondoa, kisha kutakuwa na ukhalifa juu ya njia ya utume».
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya ofisi kuu ya habari ya Hizb ut-Tahrir
Mukhlasa Al-Uzbekistania