Wadhifa ya Rais katika Asia ya Kati Inalingana na Ufalme
(Imetafsiriwa)
Habari:
Shirika la Habari la Radio Liberty liliripoti mnamo Mei 29 kwamba "Putin alifanya mazungumzo na Rustam Imam Ali, Mkuu wa Baraza la Seneti la Tajikistan. Kama sehemu ya ziara yake rasmi huko Moscow, Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Tajik (Baraza Kuu), na Meya wa Dushanbe, Rustam Imam Ali, alifanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin, Spika wa Baraza la Shirikisho Valentina Matviyenko, na Spika wa Duma Vyacheslav Volodin. Mazungumzo yalilenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, kuendeleza mazungumzo ya bunge, kupanua ushirikiano wa kibinadamu, na masuala ya uhamiaji wa wafanyikazi, kulingana na ukurasa wa Baraza la Kitaifa la Tajik kwenye Facebook.
Maoni:
Hii si ziara ya kwanza ya mwana wa dikteta Imam Rahmanov, kwenda Urusi. Mkutano huu uliashiriwa na sherehe rasmi zaidi, na ulikuwa kama onyesho. Dikteta Imam Rahmanov ana umri mkubwa, na afya yake inazidi kudhoofika, ambayo inafanya kuwa muhimu kutafuta mgombea wa urais. Asia ya Kati imekuwa, na bado iko, chini ya udhibiti wa Kremlin kwa zaidi ya miaka mia moja, na kwa hivyo madikteta wa nchi hizi huwatuma warithi wao kwa Kremlin kupata idhini au kukagua uteuzi wa wadhifa wa rais.
Tunaweza kushuhudia hali kama hiyo na mpito wa madaraka kutoka kwa dikteta wa Turkmenistan, Gurbanguly Berdimuhamedov, kwenda kwa mwanawe Serdar Berdimuhamedov. Berdimuhamedov alirithi madaraka kutoka kwa baba yake mwaka 2022. Miaka michache kabla ya hapo, Serdar alipitia hatua nyingi za mageuzi kufikia madaraka, kama vile meya wa mkoa, nyadhifa za mawaziri, na wadhifa katika Baraza la Usalama, na kadhalika. Kwa muda, baba ya Serdar alisafiri naye kwenye mikutano rasmi, kama tahadhari dhidi ya kupoteza madaraka, lakini alikuwa na hakika kwamba kila kitu kinaenda kulingana na mpango wake, hivyo Gurbanguly alimruhusu mwanawe kutoka kwa uhuru. Kwa hivyo, mamlaka ilihamishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mwana.
Tofauti na marais wa Turkmenistan na Tajikistan, marais wa Uzbekistan na Kazakhstan, wa zamani na wa sasa, wana mabinti kama warithi, ambayo inafanya mpito wa madaraka kuwa mgumu. Haikubaliki katika utamaduni wa Asia ya Kati kwa mwanamke kuwa rais wa nchi. Lakini hata hivyo, kama tulivyoona, mabinti wa madikteta wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika maisha ya kisiasa ya nchi. Sio muda mrefu uliopita, binti za Karimov na Nazarbayev walishiriki katika karibu shughuli zote za kiuchumi nchini. Leo, binti wa Mirziyoyev hashiriki tu katika siasa za ndani za nchi, lakini pia anaiwakilisha Uzbekistan nje ya nchi.
Katika historia ya kisasa ya Asia ya Kati, mila mpya imeibuka, ambayo ni kwamba yeyote anayechukua urais wa nchi huchukua mamlaka yake yote, akiwateua jamaa zake katika nyadhifa zenye ushawishi, na kuwarithisha, kama ilivyo katika mfumo wa kifalme. Mara tu madikteta wanaposhika madaraka, hawaiachi isipokuwa kwa kifo au dharura. Na wakati wao wakiwa madarakani, familia yao yote huwatesa watu kwa uonevu na dhuluma.
Sisi ni Waislamu wa Asia ya Kati, na wageni kwa mifumo isiyo ya Kiislamu ya utawala kama vile jamhuri na falme. Katika Uislamu, mamlaka ni ya Umma, na enzi kuu ni ya Sharia, si ya watu wala ya Khalifa. Na Umma unamwunga mkono Khalifa ili kutekeleza Sharia katika ardhi na kutawala kulingana na sheria ya Mungu.
Mwenyezi Mungu amesema katika Kitabu chake Kitukufu: ﴿Hukumu si ila ya Mwenyezi Mungu﴾, na akasema: ﴿Na ni nani aliye bora zaidi kuliko Mwenyezi Mungu katika hukumu kwa watu wenye yakini?﴾, na akasema: ﴿Na kwamba wahukumu baina yao kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao, na tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi ujue kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.﴾.
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisimamisha Dola ya Kiislamu huko Madina, na akatueleza njia bora za kujenga taasisi za dola. Aliwateua magavana na majaji, akachagua wasaidizi wake, na akaunda baraza la ushauri. Na ﷺ alichukua uongozi wa dola hii, na masahaba zake, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, walimwunga mkono kama mtawala. Baada ya kufariki kwake ﷺ, masahaba wema waliendeleza kazi hii, wakaitwa makhalifa, na mfumo wa utawala ni Khilafah. Na hakuna wokovu kwetu kutoka kwa watawala madhalimu ambao hawatawali kwa hukumu za Kiislamu isipokuwa kwa kufanya kazi kwa njia ya Mtume ﷺ, ili kusimamisha Khilafah Rashidah ya Pili kwa njia ya Utume, inayoongozwa na Khalifa Rashidah anayetawala kwa sheria ya Mungu, na kuondoa dhuluma na uovu, na kueneza nuru ya Uislamu katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye msaada.
Imeandikwa kwa ajili ya Radio ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir