Meloni amzungumzia Netanyahu kuhusu misaada ya Gaza na ripoti ya UM inapunguza umuhimu wa usitishaji mapigano
Habari:
Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, amemtaka Waziri Mkuu wa shirika la Kiyahudi, Benjamin Netanyahu, kuruhusu ufikiaji kamili na bila vizuizi wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. Ofisi ya Meloni ilisema katika taarifa kwamba alisisitiza katika mawasiliano na Netanyahu siku ya Jumatano, 2025/7/30, juu ya ulazima wa kusitisha mara moja uhasama kutokana na hali katika Gaza, ambayo aliielezea kuwa haivumiliki na isiyo na msingi.
Maoni:
Kwa mtazamo wa habari hii, mtu anajiuliza ikiwa mwanamke katika nafasi ya uongozi nchini Italia anamwomba mkuu wa shirika la Kiyahudi Netanyahu kuruhusu ufikiaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, basi wako wapi watawala wa Waislamu wanaodai kuwa wanaume?! Uanaume unamaanisha msimamo wa uaminifu katika shida na matatizo. Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Miongoni mwa Waumini wapo watu walio sadikisha yale waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Basi wapo walio kwisha timiza nadhiri yao, na wapo wanangojea; wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo.﴾.
Huyu hapa mtawala wa Misri, Sisi, ambaye Gaza iko umbali wa mita chache kutoka kwake, anazuia kuwasili kwa misafara ya misaada iliyotoka katika nchi mbalimbali za dunia kuvunja mzingiro dhidi ya watu wetu huko Gaza, na anafunga kivuko cha Rafah, ambacho ndicho njia pekee ya watu wa Gaza kuelekea ulimwengu wa nje, badala ya kuhamasisha jeshi lake kujibu kilio cha wanawake, watoto na wazee na kujibu kauli yake Mwenyezi Mungu: ﴿Na wakikuombeni msaada katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia﴾.
Na huyu hapa mtawala wa Jordan, wakala wa Uingereza, Abdullah wa Pili, anawakamata waandamanaji waliotaka kuvunjwa kwa mzingiro dhidi ya watu wa Gaza, na wakati huo huo anaandaa tamasha la Jarash na anatoa wito wa uchafu na hajali kinachoendelea kwa watu wa Gaza ambao wanakufa kwa njaa na mapigo.
Na huyu hapa mtawala wa Uturuki, Erdogan, analishambulia shirika la Kiyahudi kwa ulimi wake tu kuwadanganya watu wanyonge kana kwamba yeye ni mmoja wao na hana majeshi yenye nguvu zaidi katika eneo hilo, ingawa ndugu zetu nchini Uturuki, wakiwemo wanachama wa Hizb ut-Tahrir, waliandaa maandamano kote nchini na kutaka jeshi lihamasishwe kuwasaidia watu wetu huko Gaza, lakini hakuna anayesikia.
Halafu wako wapi wamiliki wa medali na vyeo katika majeshi ya Waislamu wakati wanasikia vilio vya watoto na wanawake waliodhoofishwa kutoka Gaza? Wanawezaje kufurahia maisha na watoto na wake zao? Je, hakuna miongoni mwao Salahuddin ambaye atapindua meza juu ya watawala hawa walioshindwa na kulieleza kwa Mwenyezi Mungu, na kuisaidia Hizb ut-Tahrir kuanzisha tena maisha ya Kiislamu kwa kuanzisha Khilafah kwa njia ya Utume?! Je, hakuna miongoni mwao ambaye atajiuza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kufanya biashara na Mwenyezi Mungu ili apate ushindi wa dunia na akhera?! Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Enyi mlio amini! Je, nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu chungu? Mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mpiganie Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Hiyo ni bora kwenu, lau mnajua. Atakusameheni madhambi yenu, na atakuingizeni katika Bustani zipitazo mito kati yake, na makaazi mazuri katika Bustani za milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. Na mengine mnatayapenda: Msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu. Na wabashirie Waumini.﴾.
Imeandikwa kwa Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Abdullah Abdul Hamid - Jimbo la Iraq