Uamsho wa Mataifa Huwa kwa Fikra Wala Sio kwa Dhahabu na Fedha!
Habari:
Pamoja na usiku wa kwanza wa mwaka mpya wa Hijria, nguo ya thamani kubwa zaidi ulimwenguni, nguo ya Al-Kaaba Tukufu, hubadilishwa. Hutumia takriban kilo 1,000 za hariri ghafi, kilo 120 za nyuzi za dhahabu na nyuzi 100 za fedha. Idadi ya vipande vya ukanda wa nguo ya Al-Kaaba Tukufu ni vipande 16, vipande 6 na taa 12 chini ya ukanda na Samadiyat 4 zimewekwa kwenye pembe za Al-Kaaba, pia inajumuisha vipande 47 vya hariri vilivyopambwa na aya 68, na utengenezaji wake ulichukua mwezi. Nguo hii ina uzito wa kilo 1416.
Maoni:
Hakika nguo ya Al-Kaaba, bali Al-Kaaba yenyewe, si ya thamani zaidi wala bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko damu na heshima ya Muislamu hata ipambwe kwa dhahabu, fedha na hariri na itengewe pesa hizi zote, na Waislamu wanahama na kuzingirwa bila chakula, kinywaji au dawa! Tuko katika zama za utawala wa watu wajinga wakati pesa za Waislamu zinapotea katika kutengeneza nguo ya gharama kubwa zaidi ulimwenguni, na kutengeneza sahani kubwa zaidi ya mchele kuingia kwenye Kitabu cha kumbukumbu cha Guinness cha rekodi! Hivi ndivyo umma wa Kiislamu ulivyo; majeshi bila nguvu wala jihad, pesa zinapotea, na vijana bila mustakabali, rasilimali zetu zinaporwa na kupewa kama zawadi kwa vichwa vya ukafiri ili kutengeneza silaha za kutuua nazo na kuharibu nchi zetu, kisha watawala wanatutokezea kulaani au kulia, na ndio msingi wa balaa na asili ya ugonjwa ambao umewapata Waislamu. Wakati Umar ibn al-Khattab, Mwenyezi Mungu amridhie, aliulizwa: Je! Hutaifunika Al-Kaaba kwa hariri? Akasema: "Matumbo ya Waislamu yanafaa zaidi kuliko kuifunika Al-Kaaba kwa hariri."
Hakika Makka Al-Mukarama, Nyumba ya Mwenyezi Mungu ndani yake, Waislamu hukutana kutoka sehemu mbali mbali za dunia, wanaacha dunia yao na kile wanachomiliki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hivyo unamwona Muislamu anatamani na kutarajia kwa shauku kubwa kutembelea Nyumba ya Mwenyezi Mungu, lakini Hijja na Umra zimekuwa biashara na fursa ya kukusanya pesa, kila kitu ni kwa malipo, vitu vimezidi, hata kokoto za kumtupa shetani zinauzwa!! Hakika nembo za Mwenyezi Mungu zitabaki kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ama utata tunaishi nao na kuwachukiza Waislamu ni matokeo ya kawaida ya kuacha sheria ya Mwenyezi Mungu, tumekuwa katika zama ambazo wakala, msaliti, na mtu anayeidhinisha (mahusiano na Israel) anaitwa mtumishi wa misikiti miwili mitakatifu, naye ndiye aliyeuza dini yake kwa bei rahisi zaidi ili Wayahudi na Wakristo wamridhie. Hivi ndivyo viungo vyetu vilivyokatwa na Waislamu kuzama katika ufisadi na sherehe za uchi na uovu. Amesema kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: «WATAKUJIA WATU MIAKA YA UDANGANYIFU; MWONGO HUAMINIKA NA MWENYE UKWELI HUTOKA UWONGO, MWENYE AMANA HUAMINIKA NA MWAMINIFU HUTOKA MSAFITI, NA HUZUNGUMZA RUWEYBIDHA». Akaulizwa: RUWEYBIDHA NI NINI? Akasema: «MTU MJINGA KATIKA MAMBO YA UMMA».
Dola ya Kiislamu imetoweka kutoka kwetu, kwa hivyo Uislamu hauna rangi wala harufu, kwa hivyo walitutawala kwa mfumo mbovu, wa upendeleo hadi tukawa mkiani mwa mataifa na mahali pa kila anayeinuka na kuanguka. Hivi ndivyo tulivyokuwa na bado tauni inaendelea maadamu watawala hawa wanazurura katika nchi za Waislamu. Uislamu ni kanuni; itikadi ambayo inatoka mfumo, mfumo wa kina, kamili wa ibada, shughuli, mfumo wa kiuchumi na kijamii, mahusiano ya nje na mfumo wa utawala... ﴿HATUJAPUUZA KITABUNI KITU CHOCHOTE﴾. Kwa Uislamu, waja na nchi hupanda na kuwaondoa katika mila za zamani na imani potofu, ni dini na dola na sio dini ya kikuhani iliyojikita katika nyumba za ibada na shughuli zingine.
Hakika kuondoka kwa watawala hawa vibaraka ni lazima, kwa ufahamu na utashi, umma unawatema, na kwa kuondoka kwao, wema utaenea, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na haki itashinda, na kwa mfumo wa Uislamu pekee ndio tunaondoa utawala wa madhara na kurejesha hukumu ya Mwenyezi Mungu katika ardhi, na hii ni ahadi yake, Mtukufu na Mkuu, licha ya hila za wanaofanya hila na njama za wafanya njama.
Imeandikwa kwa redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Zainab Bin Rahouma