Mfumo wa Aal Saud Unafuata Magharibi Hatua kwa Hatua kwa Kubadilisha Mipaka ya Uchi!
Habari:
Mamlaka Kuu ya Udhibiti wa Habari nchini Saudi Arabia imefichua utoaji wa kanuni mpya za udhibiti zinazolenga maudhui yanayochapishwa kupitia majukwaa ya habari na mitandao ya kijamii, katika hatua inayolenga kulinda ladha ya umma na kuimarisha maadili ya jamii... Kuhusu kanuni za muonekano wa jumla, Mamlaka iliwataka watu binafsi kuepuka kuvaa nguo zinazoonyesha mwili kutoka mabegani na kifua hadi miguuni, na ilipiga marufuku nguo zinazobana ambazo zinaonyesha maumbo ya mwili, pamoja na kuzuia kuvaa nguo za uwazi ambazo haziendani na adabu ya jumla na maadili yanayoenea. Hatua hii inakuja kama sehemu ya mwelekeo mpana wa Saudi Arabia kuelekea kudhibiti nafasi ya kidijitali na habari, ili kuhakikisha kuwa inaendana na utambulisho wa kitaifa na inalinda maadili ya kimaadili na kijamii. (Al Jazeera, 2025/09/22)
Maoni:
Inaonekana kwamba uundaji wa Mamlaka Kuu ya Udhibiti wa Habari katika nchi ya Haramain kwa sheria za habari zilizopitishwa unakuja kwa usawa na mawazo ya Magharibi kuhusu kulinda uhuru wa watu binafsi na taarifa zao za kibinafsi, na kwa usahihi zaidi, kwa namna inayofanana na sheria za Kanuni ya Jumla ya Ulinzi wa Data iliyotolewa na nchi za Umoja wa Ulaya mwaka 2018.
Je, Magharibi wanajali zaidi kuhusu mwanadamu kuliko Muumba wake?! Je, matukio ya mauaji ya kimbari huko Gaza hayakuzifichua nchi za Magharibi kwa ujumla?
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: «Hakika mtafuata nyendo za wale waliokuwa kabla yenu hatua kwa hatua, na pima kwa pima, hata kama wangeingia katika tundu la kenge, mngeliingia»; tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu; Mayahudi na Wakristo? Mtume ﷺ akasema:
«Nani basi?!» (Imesimuliwa na Masheikh wawili)
Mpaka lini watawala wa nchi ya Haramain watafuata makafiri hatua kwa hatua, na pima kwa pima? Je, uigaji huu utafikia hatua ambayo mfumo unaotawala utazingatia kwamba hakuna tofauti zozote kati ya mwanamke na mwanaume? Na kuruhusu tendo la watu wa Lut na usagaji na aina nyinginezo za upotovu kwa kisingizio cha uhuru baada ya kuachana na dhana ya mahram kwa mwanamke? Je, mfumo huu una nini katika akiba yake kwa Waislamu baada ya mshangao?
Je, mkono wa mwanamke na nywele zake hazija kuwa tena ni uchi kwa wale wanaosimamia mfumo huu? Na je, bega na kifua cha mwanaume vimekuwa uchi? Je, wanaosimamia wanafikiri kwamba makafiri watakuwa radhi nao? Basi upotevu ni upotevu na uharibifu ni uharibifu kwa kila mtu ambaye hakuchukua Uislamu kama msingi wa kiitikadi wa kuhukumu vitu, vitendo, na tabia, ikiwa ni pamoja na mikataba na sheria.
Mwenyezi Mungu ameonya dhidi ya matokeo ya kile wanachokifanya watawala wa Waislamu, wakiwemo watawala wa nchi ya Haramain, kwa kusema: ﴿Wala Mayahudi hawataridhika nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uongofu. Na kama utafuata matamanio yao baada ya kukujia ujuzi, huna mlinzi wala msaidizi mbele ya Mwenyezi Mungu﴾; Hakuna mlinzi wala msaidizi kwa yule anayefuata matamanio ya wanadamu na makafiri, bali ni hasara iliyo wazi katika dunia na Akhera.
Imeandikwa na Radio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Nizar Jamal