Uislamu ni mfumo kamili usiotenganishwa
Habari:
Hivi sasa serikali ya Syria inajitahidi kuchora upya ramani ya fedha kupitia mageuzi mapana ya kisheria na kimuundo. Gavana wa Benki Kuu alisisitiza kuwa benki hiyo, kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, imeandaa mpango wa utulivu unaodumu kati ya miezi 6 na 12, ambao unajumuisha mageuzi ya benki kuu, kurekebisha sheria za benki, kuzindua programu za ufadhili wa nyumba, kusasisha bima ya jamii, na kuchochea uwekezaji wa Wasiria nje ya nchi. Mpango huo unajumuisha kusasisha kanuni za benki ili kuhimiza zana za ufadhili wa Kiislamu, na kutangaza utoaji wa hatifungani za kwanza za Kiislamu nchini Syria, ambayo ni mbadala wa bondi za kawaida kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Serikali inatarajia kuwa hatua hizi zitachangia katika kujenga mfumo wa benki ulio bora zaidi na huru, unaoweza kusaidia juhudi za ujenzi na kuvutia mitaji kutoka nje ya nchi, huku ikiimarisha uwazi na kuboresha ubora wa data, kwa mujibu wa viwango vya kimataifa. (Al Jazeera)
Maoni:
Ikiwa watu wa Syria wanaamini kuwa sheria za Kiislamu ndizo sheria pekee zinazofaa kutumika na kuzifuata, na kwamba Uislamu ndio suluhisho la kweli kwa matatizo yao yote, kwa nini serikali ya Syria haitumii Uislamu kikamilifu? Kwa nini inajaribu na kufanya kazi ya kupitisha suluhisho za kiuchumi za kibepari huku ikizivalisha nguo za Uislamu "benki za Kiislamu", "hatifungani za Kiislamu"...?!
Kutosheka na viraka, hata wakidai kuwa vinatoka katika Uislamu, hakutatua chochote, kwani asili, ambayo ni mfumo wa kibepari, ikiwa imeharibika, basi kinachotokana nayo kitakuwa kibaya. Tumeona majaribio kadhaa katika nchi za Waislamu ambazo zilifuata njia hiyo hiyo na hazikufanikiwa, bali ziliongeza kina cha mzozo wa kiuchumi. Kwa upande mwingine, Uislamu lazima uchukuliwe wote kama itikadi na mfumo na hauwezi kugawanywa au kunukuliwa kutoka kwake.
Kwa hivyo, ilikuwa juu ya serikali ya Syria kutumia Uislamu kwa ukamilifu, na sio kunukuu baadhi ya hukumu zake kutoka hapa na pale na kuzipotosha ili kuziunganisha ndani ya mfumo mchafu wa kibepari ambao uovu wake umeonekana, na kushindwa kwake kumefichuliwa.
Imeandikwa na Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Nadhir Bin Swaleh - Wilaya ya Tunisia