Nguvu Zetu Ni Neema, Lakini Mgawanyiko Wetu Ni Laana
(Imetafsiriwa)
Habari:
Pentagon: Marekani haitaki kwenda vitani na Iran baada ya kushambuliwa kwa maeneo matatu ya nyuklia. (AP News)
Maoni:
Pentagon inasema kwamba Marekani haitaki kwenda vitani na Iran; baada ya kudondosha mabomu kumi na nne ya kupenya ngome kwenye vituo vitatu vya nyuklia vilivyo ndani kabisa ya ardhi ya Iran! Tamko kama hili sio unafiki tu, bali ni jambo la kuchukiza. Ni mfano wa fikra za kikoloni za kiburi. Mtu mwenye akili anawezaje kuamini kwamba vita sio nia, wakati nchi inafanya mashambulio ya kuratibiwa dhidi ya nchi nyingine?!
Lakini kinachokasirisha zaidi kuliko udanganyifu wa utawala huu, ni ukimya wa ulimwengu na kutokuwa na uwezo mbele ya uchokozi huu wa wazi. Operesheni ya hivi karibuni ya Amerika, iliyopewa jina la "Operesheni Nyundo ya Usiku wa Manane," sio ushahidi wa nguvu ya Amerika, lakini ni ufunuo wa aibu wa ukweli wa kutokuwa na uwezo wa kisiasa na mgawanyiko ambao unaharibu mwili wa taifa la Kiislamu. Sio kwa sababu taifa linakosa njia za kutetea haki zake, lakini kwa sababu nia imetawanyika katika mipaka iliyokatwa, inayoongozwa na mifumo ambayo wasiwasi wake wa kwanza ni kuhifadhi viti vyao vya enzi, na uaminifu wao kwa Washington kabla ya watu wao.
Pentagon ilijigamba hadharani kwamba ndege za kivita za Amerika ziliingia anga ya Iran bila kugunduliwa! Tukio hili linapaswa kuwa wakati wa kutafakari kwa kina na uwajibikaji mzito. Taifa la Kiislamu linaenea katika mabara, linamiliki utajiri mkubwa, linadhibiti njia za bahari za kimkakati, na linajumuisha baadhi ya majeshi makubwa zaidi ulimwenguni. Hata hivyo, uwezo huu mkubwa umepooza; sio kwa sababu ya nguvu ya adui, lakini kwa sababu ya kukosekana kwa umoja wa kisiasa na uongozi ambao unawakilisha watu kweli.
Mwenyezi Mungu ameipa neema taifa hili na vipengele vyote vya mamlaka, maendeleo, na uongozi wa ulimwengu. Hata hivyo, rasilimali zetu zinasalia zimetawanyika, na majeshi yetu yamefungwa na mipaka bandia. Mashambulio kwenye vituo vya Fordo, Natanz na Isfahan sio mashambulio tu ya kimbinu, bali ni ujumbe wa wazi wa ishara; ni ujumbe unaolenga kila mfumo katika nchi za Waislamu: jisalimishe, achana na silaha zako, jadili masharti yetu, au ukabiliane na uharibifu!
Kwa hivyo, wito wa mfumo wa kisiasa wa Kiislamu; Khilafa, kurejesha haki, usawa na huruma kwa wanadamu, kama ilivyofanya hapo awali, sio ndoto tu, bali ni wajibu, ni lazima, na ni njia pekee inayowezekana kuelekea siku zijazo. Khilafa itaunda upya mizani ya nguvu za ulimwengu, na kurudisha taifa kuwa taifa bora zaidi lililoletwa kwa watu, likichukua ujumbe wa Mungu kwa wanadamu wote.
﴿Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa na woga na ikaondoka nguvu yenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.﴾
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Haitham bin Thabit
Mwakilishi wa Habari wa Hizb ut-Tahrir huko Amerika