Majibu ya Watawala Wetu Hayafikii Kiwango cha Matarajio ya Umma
Habari:
Waziri Mkuu wa Shirika la Kiyahudi Benjamin Netanyahu, wakati wa mahojiano ya televisheni na kituo cha Kiyahudi cha "i24", alitoa matamshi yenye utata aliposema: (Mimi niko kwenye misheni ya kihistoria na kiroho na nimeunganishwa kihisia na maono ya "Israeli Kuu") (Al-Jazeera Net, kwa muhtasari)
Na chini ya kichwa (Ulaani wa Kiarabu kwa matamshi ya Netanyahu kuhusu "Israeli Kuu" na Misri inaomba ufafanuzi) iliandika Al-Jazeera Net: Saudi Arabia, Qatar, Jordan, Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Jumatano hii, zimelaani matamshi ya Netanyahu kuhusu kile anacho kiita "maono ya Israeli Kuu", na kuieleza kama uvamizi wa uhuru wa nchi za Kiarabu.
Maoni:
Hivyo ndivyo watawala wajinga katika nchi yetu walivyozoea: kujibu matamshi na vitisho vya maadui kwa kulaani, kukemea, kulaumu na kukataa, umma haujazoea kutoka kwao vitendo ambavyo vinafikia kiwango cha tukio au vitisho, na hii inamaanisha kuwa wao wako katika bonde na umma uko katika bonde lingine, na kwamba masuala ya umma hayawahusu kwa vyovyote vile, na kwamba suala lao linatofautiana na masuala ya umma, bali linapingana nayo.
Suala kuu la umma ni kutawala kwa kile ambacho Mungu amekiteremsha, na kuunganisha vyombo hivi vya kibonzo vilivyopo katika nchi yetu chini ya bendera ya ukhalifa, ili kurudi katika hali yake ya zamani kama ilivyokuwa kwa zaidi ya karne kumi na mbili; umma mtukufu kwa Uislamu, unaotawala kwa Uislamu, na kuubeba kama ujumbe wa uongozi na rehema kwa watu wote, umma mtukufu na wa kuheshimika, hakuna yeyote kati ya maadui zake anayethubutu kusema neno linalouchafua au ardhi yake, achilia mbali kuthubutu kufanya kitendo chochote kinachouathiri au kuathiri ardhi yake. Ama suala la watawala wetu leo ni kulinda viti vyao vilivyochakaa, na kulinda maslahi ya mabwana zao katika nchi za kikafiri, na badala ya kuwalinda umma na maslahi yake, wanalinda maslahi ya maadui na mipaka yao, na wanawakabidhi wana wa umma kwa maadui zake.
Imebainika kwa kila mwenye macho kwamba msiba wa umma wa Kiislamu uko kwa watawala wake, na kwamba watawala hao ndio sababu ya matatizo yake yote, na hakuna suluhisho kwa matatizo hayo ila kuwaondoa, na kuanzisha dola ya Kiislamu; dola ya ukhalifa kwa njia ya unabii, ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alitoa habari njema, na ambayo Hizb ut-Tahrir inafanya kazi kuianzisha, na wakati huo Netanyahu na wale walio nyuma yake kutoka kwa viongozi wa nchi za kikafiri watajua ukweli wa Waislamu ﴿NA WALE WALIO DHULUMU WATAJUA MAGEUKO GANI WATAGEUKA﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Khalifa Muhammad - Wilaya ya Jordan