Rais wa Colombia Atoa Wito wa Kuanzishwa Jeshi la Ukombozi wa Palestina
Habari:
Rais wa Colombia Gustavo Petro katika hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano tarehe 2025/09/24 alitoa wito wa kuanzishwa jeshi la kimataifa la ukombozi wa Palestina, na Petro alisema "Ni lazima kwa nchi za kusini mwa ulimwengu ambazo hazikubali mauaji ya kimbari, kuunda kikosi cha silaha kwa ajili ya kutetea maisha ya watu wa Palestina, na kujitetea dhidi ya ukatili na ubabe unaoenezwa na Amerika na Jumuiya ya Kijeshi ya Atlantiki ya Kaskazini "NATO", na Petro aliongeza: "Tunahitaji jeshi kutoka kwa nchi ambazo hazikubali mauaji ya kimbari, kwa hivyo ninazitaka nchi za ulimwengu, kama sehemu ya ubinadamu wao, kuunganisha silaha na majeshi. Ni lazima tukomboe Palestina".
Maoni:
Rais wa Colombia amesema kile ambacho hakuna mtawala yeyote kati ya watawala wa nchi za madhara katika nchi za Waislamu anayethubutu kusema hata sehemu ya kumi yake, kwani mtu huyo anatambua kuwa janga ambalo watu wa Palestina wanaishi haliwezi kutatuliwa isipokuwa kijeshi na kuhamasisha majeshi kwa ajili ya ukombozi wake, kwani uvamizi hautoweki ila kwa nguvu, vipi ikiwa uvamizi huu unaungwa mkono na nchi zote za ulimwengu, haswa kutoka Amerika na Ulaya, ambazo zinazipa silaha, pesa na wataalam ili kuua, kuharibu na kuangamiza mazao na vizazi bila hesabu au usimamizi?
Rais wa Colombia anazungumza kutoka jukwaa la Umoja wa Mataifa mbele ya marais wa nchi za ulimwengu kwa ujasiri wote na kunguruma kama simba bila kujali mtu yeyote kwamba yuko tayari kutoa wanajeshi 20,000 wa Colombia kuchangia katika ukombozi wa Palestina, wakati watawala wa Waislamu, Mwenyezi Mungu awaangamize, wamejitolea kukaa kimya wakiwa wamefunikwa na aibu, fedheha na unyonge, wakitosheka na hotuba za kulaani na kukemea kana kwamba utawala wa Kiyahudi unawajali na kulaani kwao na kukemea kwao, na ukatili umefikia kilele chake wakati rais wa Indonesia alipotoa hotuba yake akisema: "Ni lazima tutambue, tuheshimu na tuhakikishe usalama na usalama wa (Israeli), ni hapo tu tunaweza kupata amani ya kweli", na akamalizia maneno yake na "Shalom"! Jambo la kushangaza sana, kwamba rais wa Colombia ambaye si Muislamu anatoa wito wa chaguo la kijeshi la kutatua suala la Palestina, wakati watawala wa Waislamu bado wako katika upotovu wao wa zamani wakitafuta amani ya kudhalilisha na utawala wa Kiyahudi baada ya kushambulia Lebanon na Syria na kukalia sehemu zao na kuharibu Gaza kabisa!!
Msimamo unaokinzana kuhusu Palestina kati ya baadhi ya serikali za Magharibi na watawala wa Waislamu haukuishia katika msimamo huu, kwani hapa Uhispania inafuta mkataba na utawala wa Kiyahudi wenye thamani ya euro milioni 700 kwa ajili ya kununua virusha roketi, na pia ilifuta mkataba mwingine unaojumuisha virusha roketi 168 vya kuzuia vifaru vyenye thamani ya euro milioni 287, na tarehe 2025/09/29 tovuti ya Al Jazeera Net ilisema kwamba gazeti la Uhispania la Albayis lilifichua kwamba Uhispania ilizuia kupita kwa ndege na meli za Marekani zilizobeba silaha, risasi na vifaa vya kijeshi vilivyokuwa vikienda kwenye utawala wa Kiyahudi kupitia kambi mbili za kijeshi huko Cadiz na Seville, na upande mwingine tunapata kwamba Firauni wa Misri, Sisi, alisaini mkataba na utawala wa Kiyahudi tarehe 2025/08/07 wa kununua gesi yenye thamani ya dola bilioni 35! Na huku maandamano na mikesha ikizunguka mitaa ya Ulaya ikidai kusimamishwa kwa mauaji na vita vya mauaji ya kimbari huko Gaza, tunapata kwamba serikali za Kiarabu haziruhusu maandamano yoyote ya mshikamano na Gaza, lakini jeshi la Jordan lilifyatua risasi mnamo 2025/09/28 dhidi ya watu wawili waliokaribia mipaka ya Jordan na Palestina, ambayo ilisababisha vifo vyao!
Milango ya suluhu kwa tatizo lolote linalowakabili Waislamu leo imefungwa kwa sababu ya watawala hawa vibaraka, na haihitaji kusema kwamba hakuna ufufuo au maendeleo ila kwa kuondoka kwao, kwani wameharibu umma na kuukandamiza katika miaka yote ya utawala wao mkali kwa miaka mia moja au zaidi, na suluhisho linajulikana kwa kila Muislamu, ambayo ni kuweka Uislamu katika nafasi ya utekelezaji, je, Waislamu watahamasika kuwaondoa watawala hawa wahalifu na kumwapisha Khalifa awe miongoni mwao kama alivyosema Mtume ﷺ «Hakika Imamu ni ngao anapiganwa nyuma yake na anaogopwa», ili aongoze umma mzima kukomboa Kibla cha kwanza na Haram ya tatu na kuirejesha katika himaya yake tena?
Imeandikwa kwa Radio ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Muhammad Abu Hisham