Kufuata Misingi ya Mahakama ya Kimagharibi
Al-Burhan Amteua Wahbi Kuwa Rais wa Mahakama ya Kikatiba!
Habari:
Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, leo alitoa amri ya kikatiba, iliyoamuru kumteua Dkt. Wahbi Muhammad Mukhtar kuwa Rais wa Mahakama ya Kikatiba, na Mkuu alielekeza mamlaka husika katika serikali kutekeleza uamuzi huo. Uamuzi huo unatokana na pendekezo la Tume ya Kitaifa ya Utumishi wa Mahakama. (Shirika la Habari la Sudan (SUNA), 2025/8/30)
Maoni:
Hakika, mahakama katika Uislamu ni kutoa habari ya hukumu ya kisheria kwa njia ya lazima, nayo hutatua mizozo kati ya watu, au huzuia kile kinachodhuru haki ya jamii, au huondoa mzozo unaotokea kati ya watu na mtu yeyote aliye katika chombo cha utawala; watawala au wafanyakazi, Khalifa au yeyote aliye chini yake, na kwa hivyo, kuna majaji watatu; mmoja wao ni hakimu ambaye anasimamia utatuzi wa mizozo kati ya watu katika miamala na adhabu, wa pili ni msimamizi ambaye anasimamia utatuzi wa ukiukwaji unaodhuru haki ya jamii, na wa tatu ni hakimu wa malalamiko ambaye anasimamia kuondoa mzozo unaotokea kati ya watu na serikali.
Inawezekana kuwa na viwango vingi vya mahakama kuhusiana na aina za kesi; inaruhusiwa kuwateua baadhi ya majaji kwa ajili ya kesi maalum hadi kiwango fulani, na kuamuru kesi zingine kwa mahakama zingine, lakini hakuna mahakama ya kikatiba au mahakama kuu, na pia hakuna mahakama za rufaa, au mahakama za uamuzi. Hukumu kutoka upande wa uamuzi wa kesi ni kiwango kimoja, kwa hivyo, hakimu anapotamka hukumu, hukumu yake itatekelezwa, na hukumu ya hakimu mwingine haibatilishi kabisa isipokuwa ahukumu kinyume na Uislamu, au kukiuka maandishi yaliyokatwa katika Kitabu au Sunnah au makubaliano ya Masahaba, au ikidhihirika kuwa alihukumu hukumu kinyume na ukweli halisi. Na yule aliye na mamlaka ya kubatilisha hukumu hizi ni hakimu wa malalamiko.
Hii ndiyo mfumo wa mahakama katika Uislamu, na kwa hivyo hakuna kesi zinazosubiri kwa miezi au miaka bila kutatuliwa kama inavyotokea chini ya mahakama hii ya kimagharibi, ambapo hakimu anahukumu kesi, kisha inahamishiwa kwenye rufaa, kisha mahakama kuu, kisha mahakama ya kikatiba! Na hivyo kesi zinaendelea kusubiriwa kwa miaka bila kutatuliwa, hivyo haki, heshima, na damu hupotea, na kesi zinarundikana kwa mamia katika mafaili ya mahakama...
Hivyo, tunaona daima kwamba mifumo hii ya kimagharibi ya kidemokrasia inafanya maisha kuwa magumu, na inaongeza mateso ya watu... Hii ni katika hali halisi, lakini kutoka upande wa sheria, ni haramu kuhukumu kinyume na yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyateremsha. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: ﴿Na wale wasiohukumu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyateremsha, hao ndio madhalimu﴾, na anasema: ﴿Je, huwaoni wale wanaodai kuwa wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako wanataka kwenda kupata hukumu kwa Taghuti, hali wameamrishwa wamkufuru? Na shetani anataka kuwapoteza upotevu mbali﴾, na Mwenyezi Mungu Mkuu anasema: ﴿La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye hakimu katika yale wanayozozana﴾.
Kwa hivyo, ili tuishi kwa amani na utulivu, ni lazima kutekeleza Uislamu katika mifumo yote ya maisha, ikiwa ni pamoja na mfumo wa mahakama, na hii haitatokea isipokuwa chini ya dola ya Uislamu; Ukhalifa Uliyoongoka wa Pili kwa njia ya Utume, ulio karibu kusimamishwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Imeandikwa kwa ajili ya Redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan