Uanzishwaji na Uvunjaji wa Vyama vya Siasa katika Uislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza, siku ya Ijumaa, kupiga marufuku harakati ya Labbaik Pakistan, ikisema kwamba Serikali ya Shirikisho ina "sababu za msingi" za kuamini kwamba chama hiki cha kidini cha kisiasa kinahusishwa na ugaidi. (Kiungo cha habari)
Maoni:
Mapinduzi ya 1857 yalikuwa mfano kwa watu wa bara dogo la India kuwatahadharisha dhidi ya uasi dhidi ya wamiliki wa mamlaka. Waingereza waliweka mfano huu, lakini hadi leo, watawala wanaendelea kuufuata. Tangu kabla ya kuanzishwa kwake, Pakistan imekuwa ikihusika katika mzozo unaoendelea kati ya mawazo ya kitaifa na kidini. Kabla ya kugawanywa kwa bara dogo la India, chama cha Indian National Congress kiliibuka kama mwakilishi wa watu wote wa India. Hata hivyo, ilidhihirika haraka kwamba viongozi wake walikuwa wakifanya kazi hasa kuunda serikali iliyotawaliwa na Wahindu, huku wakiionyesha kama harakati ya kitaifa. Viongozi wa Kiislamu kama vile Muhammad Ali Jinnah, Muhammad Ali Johar, Maulana Abu al-Kalam Azad, na Hussein Shahid al-Suhrawardi walifanya kazi na chama hiki kwa sababu dhana ya kujitenga haikuwahi kuonekana kama suluhisho na waliamini katika bara dogo lililounganishwa kama walivyoliona kila wakati.
Lakini baada ya muda, waligundua kuwa chama cha Congress kilikuwa kinahudumia maslahi ya Wahindu hasa, huku kikiwapuuza Waislamu. Katika kukabiliana na hili, chama kipya kiliundwa ili kulinda haki za Waislamu, ambacho ni Jumuiya ya Waislamu Wote wa India. Chama hiki kilikuwa matunda ya akili ya mwanadamu, ambayo ilitoa ufafanuzi wake maalum wa kuishi na ufufuo wa Waislamu. Uislamu unasema kwamba mawazo yote lazima yajengwe juu ya itikadi ya Kiislamu. Mkataba huu ulisababisha suluhu isiyo kamili, ambayo si ya Uislamu wala ya ulimwengu wa kisasa. Takriban miaka 40 baada ya kuanzishwa kwake, Jumuiya ilifikia lengo lake kuu, ambalo ni kuanzisha nchi huru kwa Waislamu wa India. Mwishowe, mawazo ya kitaifa yalitawala, lakini yalifunikwa na hisia za kidini ili kupata msaada wa wakazi wa Kiislamu.
Sisi Waislamu wa Pakistani tunateseka hadi leo kutokana na kujitiisha kabisa kwa fikra za kitaifa. Hisia za Kiislamu zilizorithiwa zimejikita ndani yetu kiasi kwamba hazituruhusu kuandamana kwa ajili ya Palestina, ambayo inaongeza nafasi ya kunyonywa. Kwa kuwa siasa ni uangalizi na kujali masuala ya umma, chama cha siasa katika Uislamu ni mkusanyiko wa kundi la waumini kwa msingi wa Uislamu, ambao ni wema wote, na wito kwake kama itikadi ya kisiasa na mfumo unaotawala maisha.
Kuhusu vyama vya siasa, rasimu ya katiba iliyoandaliwa na Hizb ut-Tahrir inasema yafuatayo: "Waislamu wana haki ya kuanzisha vyama vya siasa kuwawajibisha watawala, au kufikia madaraka kupitia umma, mradi tu iwe kwa msingi wa itikadi ya Kiislamu, na kwamba hukumu zinazokubaliwa ziwe hukumu za Kiislamu. Uanzishwaji wa chama hauhitaji leseni, na kila muungano usio wa Kiislamu ni haramu." Pia, hairuhusiwi kundi lolote la Waislamu kujengwa kwa msingi mwingine wowote isipokuwa Uislamu kama itikadi na mfumo. Wakati kulingana na Ibara ya 17 ya Katiba ya Pakistan, kila mtu ana haki ya kuunda vyama au vyama vya wafanyakazi, kwa kuzingatia vikwazo vyovyote vya busara vinavyowekwa na sheria kwa maslahi ya uhuru au uadilifu wa Pakistan, utulivu wa umma au maadili.
Msako wa hivi majuzi dhidi ya Harakati ya Labbaik Pakistan chini ya Sheria ya Kupambana na Ugaidi, na kupigwa marufuku kwake, unaonyesha kuwa vigezo vya serikali ya Pakistani kwa chama cha siasa vinatofautiana na vigezo vya Uislamu. Harakati ya Labbaik Pakistan ni kundi la kisiasa, kama vile makundi mengine ya kidini ya kisiasa, lilishiriki katika uchaguzi na linashikilia kiti katika Baraza, ambayo inaonyesha kujisalimisha kwake kwa mfumo na kupingana na dhana ya chama cha siasa katika Uislamu.
Kwa hivyo, matibabu ambayo harakati ilipokea yanatokana na mfumo ambao wameutambua na kuukubali kwanza na kisha kuukosoa baadaye, na kwa hivyo, katika kukabiliana na maandamano dhidi ya sera ya serikali kuhusu Palestina, wafuasi wake ambao walichukua mitaa walitendewa sawa na waandamanaji katika uasi wa 1857. Hii inaonyesha hisia za Uingereza zilizorithiwa zinazoshikiliwa na uongozi leo. Hii inaonyesha kwamba tatizo liko katika kipengele cha kidini. Mara tu itakapojaa kikamilifu na siasa za maslahi ya kitaifa, itakubalika kwa serikali. Ikiwa Harakati ya Labbaik Pakistan leo itaacha mtazamo wa kidini, hata ikiwa itabaki na jina lake kama lilivyo, haitakuwa na madhara kwa watawala wa Pakistan.
Vyama vya siasa haviruhusiwi kushiriki katika utawala wa kilimwengu ambao unamwondoa Uislamu madarakani, wala kwa kuunda serikali au kushiriki ndani yake, Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Na wasio hukumu kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio wapotovu﴾.
Hali nchini Pakistan leo inahitaji suluhu ambayo ilihitajika karne moja iliyopita, si kwa kuibuka kwa Jumuiya ya Waislamu Wote wa India, wala kwa kutoweka kwa Harakati ya Labbaik Pakistan leo, bali kwa kurudi kwenye mizizi ya Uislamu, na kukabidhi nchi kwa Khalifa, ambaye hatatoa hukumu isipokuwa kwa amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuagiza vikosi vyake kukomboa ardhi ya Al-Quds kutoka kwa makucha ya Mayahudi. Wakati huu unaweza kuwa hatua ya mabadiliko kwa Waislamu kurudi kwenye utambulisho wao wa pamoja uliokita katika Uislamu, utambulisho unaovuka mipaka, makabila na lugha.
Mwenyezi Mungu anasema: ﴿Hakika huu ni umma wenu, umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu, basi niabuduni Mimi﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya ofisi kuu ya habari ya Hizb ut-Tahrir
Ikhlaq Jehan