Gharama ya Utegemezi kwa Nchi za Kiislamu
Habari:
Waziri Mkuu wa Misri, Mustafa Madbouly, alieleza, wakati wa mkutano katika Umoja wa Mataifa kuhusu suluhisho la mataifa mawili, kwamba "Misri itakuwa mwenyeji, mara tu itakapofikiwa usitishaji wa mapigano, wa mkutano wa kimataifa wa kujenga upya Ukanda wa Gaza, kukusanya fedha zinazohitajika kwa mpango wa Kiarabu na Kiislamu wa ujenzi upya".
Maoni:
Vita vya Gaza vinapokaribia kukamilisha mwaka wake wa pili na uhalifu wa Wayahudi unapoonekana kwa ulimwengu, dalili za kumalizika kwa vita zimeanza kuonekana na nchi za Kiislamu zimeanza kujiandaa kutekeleza mpango wa ujenzi mpya wa Gaza kutoka kwa pesa za Waislamu katika hali inayojirudia, na mfano wa karibu zaidi ni vita dhidi ya Gaza mwaka 2014, ambapo watawala wetu wasaliti walishuhudia ukatili wa Wayahudi huku hawachukui hatua yoyote, mpaka Wayahudi walipomaliza, walitoka kutekeleza mipango ya ujenzi na si kudai Wayahudi kulipa gharama ya matendo yao, bali wanalipa kutoka kwa utajiri wa nchi za Kiislamu ambao mwingi unaenda kwa Magharibi kafiri mkoloni, na kile kinachotubakia cha makombo, kinalipwa kulipia gharama ya uhalifu wa Wayahudi na watawala wetu wanafurahi kumalizika kwa vita na wanaona hii ni ushindi na kwamba mazungumzo yamefanikiwa kumaliza vita, ingawa mhalifu hajawajibishwa hata kwa uharibifu wa majengo, achilia mbali mateso yaliyodumu kwa miaka miwili na roho zilizopotea.
Kulingana na mpango uliowekwa na serikali ya Misri mnamo Machi 2025, gharama ya ujenzi mpya wa Gaza inakadiriwa kuwa dola bilioni 53.2, ambayo ni gharama kubwa inayoonyesha ukubwa wa uharibifu usio na kifani, na hakuna mtu mwenye akili anayeweza kujitolea kushiriki katika kulipa kiasi hiki kwa hiari yake mwenyewe akijua kuwa mhalifu hatashiriki chochote, lakini watawala wetu hawana uamuzi wao wenyewe, wanaharakisha kutekeleza amri za Magharibi kafiri mkoloni ambaye anataka eneo hilo litulie ili kulinda ushawishi wake, na ama Wayahudi wanajua hilo na wameharibu Gaza na wanajua kuwa kuna watawala vibaraka ambao watawachukulia mzigo wa uhalifu wao.
Watawala wetu ambao walitoa trilioni za dola kwa Trump huku wakiwa wanyenyekevu kulinda nyadhifa zao wamesimama tayari kupokea amri kutoka Magharibi ya kujenga upya Gaza, na hakuna hata mmoja wao atakayethubutu kudai Wayahudi washiriki hata kwa dola moja, wao ni vibaraka waliopandwa na Magharibi ndani yetu ili kuwapa pesa zetu kwenye sahani ya dhahabu, kwa hivyo hakuna suluhisho ila kuondoa vichwa hivi ambavyo vimeinama kwa adui yetu na kurejesha dola yetu, dola ya Kiislamu; dola ya Khilafa Rashidah kwa njia ya Utume.
﴿Ikiwa Mwenyezi Mungu atakunusuruni, basi hakuna atakayewashinda; na ikiwa atakuachilieni, ni nani basi atakayekunusuruni baada yake? Na kwa Mwenyezi Mungu ndio wamtegemee Waumini.﴾
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Abdul Rahman Shaker – Wilaya ya Misri