Hiyo ndiyo hadithi yenu enyi Waislamu kwa kukosekana kwa Khilafa na Khalifa!
Habari:
"Kijiji cha Wad Al-Noura, katika jimbo la Al-Jazira katikati mwa Sudan, kilivamiwa kikamilifu katika siku moja, na zaidi ya watu 400 waliuawa, na ulimwengu haukujua hilo kutokana na kukata mawasiliano na kukandamiza sauti za raia na wanahabari." Hivyo ndivyo mwanaharakati wa Sudan, Rawan Shahin, alivyozungumza kuhusu kile Sudan inakumbana nacho kwa nguvu, kutokana na matukio mabaya. (Arabi21)
Maoni:
Hii hapa Sudan inarudi kwenye mandhari baada ya kasi ya uvamizi wa dada yake Gaza Hashim kupungua. Hii hapa Sudan iliyojeruhiwa inarudi ili sauti yake ipaze baada ya adui yetu kuitawala na kutawala mandhari yake, kwa hivyo akawashtua Waislamu ili wauane, ili turudi kwenye ujinga wetu wa kwanza. Mwenyezi Mungu amesema: ﴿Kisha nyinyi mwauana na kuwatoa baadhi yenu kutoka makwao﴾, je, mnaridhika na hili enyi Waislamu? Je, mataifa ya ukafiri yanatukusanyika katika kumwaga damu yetu, na badala ya kupigana nao na kuelekeza bunduki zetu kwao, tunazielekeza kwenye vifua vyetu?! ﴿Na tulipochukua ahadi yenu, msitamwage damu yenu wala msitoane kutoka makwao, kisha mkakiri nanyi mnashuhudia﴾.
Mwenyezi Mungu ameandika kwamba tunaishi katika zama hizi ambazo tunashuhudia mataifa ya ukafiri yakiushambulia umma wa Kiislamu kutoka mashariki hadi magharibi bila msimamizi wala mwangalizi. Mwenyezi Mungu ameandika kwamba tunaishi katika zama hizi ambazo zinafanana na zile zama ambazo umma wa Kiislamu uliishi, na mikono ya makafiri inawashambulia na kumwaga damu yao, bali ubaya na ukali wake umezidi zama hizo. Je, hamtafuata njia ya watu wakuu na kuandika historia kwa mikono yenu kama walivyoifanya ili mpate utukufu wa dunia na radhi za Mwenyezi Mungu Akhera kwa idhini yake?
Enyi Waislamu katika Sudan mpendwa: Je, hakuna mtu miongoni mwenu aliye na akili timamu kusimamisha mauaji haya na kupata heshima kubwa na kuigeuza mitihani hii kuwa zawadi kwa kuwakusanya Waislamu waliotawanyika na kusimamisha umwagaji wa damu yenu bila haki na kusimama mbele ya mipango ya ukafiri na njama zao, ili astahili radhi za Mwenyezi Mungu na watu wote kwa ujumla?!
Enyi Waislamu kila mahali: Hii ndiyo hali yenu kwani mlipewa amri na watawala wa dhiki, wakaharibu hadhi yenu baada ya utukufu na kuwadhalilisha baada ya heshima. Mtume ﷺ amesema: «Uaminifu ukitoweka, basi ngojea saa» Akaulizwa: Uaminifu unatowekaje ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: «Mambo yatakapokabidhiwa kwa wasiostahiki, basi ngojea saa» Imesimuliwa na Bukhari.
Enyi Waislamu: Hii ndiyo hali yenu, na sababu ya hilo iko mbele ya macho yenu, nayo ni kukosekana kwa Khilafa ambayo hairuhusu hilo kamwe, je, hamjiokoi kutoka katika dhiki ya dunia na adhabu ya Akhera na kufanya kazi ya kuwavua nguo wanafiki wa zama hizi ili mpate utukufu wa dunia na ushindi Akhera?!
﴿Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye litakalo kuishieni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu huingilia baina ya mtu na moyo wake, na kwamba kwake Yeye mtakusanywa﴾
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Abdullah Abdul Rahman
Mkurugenzi wa Idara ya Machapisho na Hifadhi katika Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir