Trump na Amani Kupitia Nguvu
Habari:
Trump alisema katika hotuba yake kwa maafisa wakuu wa jeshi la Marekani: "Tutalitatua tatizo la Mashariki ya Kati, ambalo kwa kweli ni jambo gumu sana." Aliongeza: "Tutakuwa tukifuatilia sehemu tete ya dunia katika Mashariki ya Kati na tutafanya kazi ya kuiweka shwari ili jeshi la Marekani lisilazimike kuingilia kati." (RT, 2025/9/30)
Maoni:
Amerika imewakusanya maafisa wake wakuu wa jeshi kutoka sehemu zote walipo ulimwenguni, baada ya Pentagon kuiita Wizara ya Vita, ikiashiria utayari wake wa vita bila mtu yeyote kujua Amerika itapigana wapi, je, ni Ukraine, Iran au Palestina, kulazimisha kile Trump anaita amani kupitia nguvu.
Wakati Trump anakubali kuwa eneo la Kiislamu ni sehemu tete ya dunia kwa sababu anaona watu wake wanachemka na hawaridhiki na watawala wao wasaliti, na wanajiandaa kupindua utawala wa Amerika na kuifukuza sio tu kutoka eneo la Kiislamu, lakini kutoka ulimwenguni kote, anajaribu kutishia.
Kiwango cha kina cha udhaifu wa Magharibi mbele ya Waislamu kimefikia hatua ambapo jeshi la Wayahudi, ambalo ni mstari wake wa kwanza wa mashambulizi dhidi ya Waislamu, limekuwa likipigana kwa miaka miwili katika Ukanda wa Gaza, eneo dogo sana kijiografia, lakini licha ya msaada wote wa Amerika na silaha, vifaa, wataalam na ushawishi wa kisiasa wa kimataifa, halijafikia malengo yake licha ya uharibifu mkubwa na mauaji.
Na ikiwa Trump alisema kuhusu jeshi la Urusi kwamba lilikuwa "chui wa karatasi" kwa sababu halikuweza kumaliza vita nchini Ukraine katika wiki moja, na inaendelea kwa miaka, anatambua kikamilifu kuwa Magharibi yote pia ni "chui wa karatasi" kwa sababu haikuweza kumaliza vita huko Gaza pia, licha ya msaada wote wa Magharibi na njama za watawala wa Kiislamu.
Mpango wa Trump wa kusafisha suala la Palestina unajumuisha mabadiliko ya ishara kwa utawala wa taasisi ya Kiyahudi kwa Gaza kwa utawala wa makafiri wengine, ambao ni Rais wa Amerika na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, wakitegemea kundi la watawala wa Kiislamu kulazimisha nguvu ya kimataifa ambayo itavunja silaha za Gaza ambazo zinawatisha, ingawa zote ni chini ya silaha ndogo.
﴿Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi juu ya jambo lake, lakini watu wengi hawajui﴾
Imeandikwa na Idhaa ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Bilal Al-Tamimi