Trump Awaita Viongozi wa Nchi 6 kwa Mkutano Kuhusu Vita dhidi ya Gaza
Habari:
Kituo cha 12 cha Kiyahudi kiliripoti, Jumapili jioni, kwamba Rais wa Marekani Trump amewaita viongozi wa Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Misri, Jordan na Uturuki kwenye mkutano kuhusu vita vya Gaza. Kituo hicho cha Kiyahudi kilisema, kikinukuu vyanzo viwili vinavyofahamu suala hilo, kwamba mkutano huo utafanyika pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumanne.
Kulingana na vyanzo hivyo viwili, mkutano huo unakuja siku chache kabla ya Waziri Mkuu Netanyahu kufika Ikulu ya White House kukutana na Rais Trump.
Maoni:
Je, si jambo la kusikitisha na la kuhuzunisha kwamba Rais wa Amerika anawaita watawala wa Waislamu na wanaitikia, na anawaamuru na wanatii?! Je, si aibu kwamba wanamngojea Trump, adui wa Uislamu na Waislamu, awaite kwenye mkutano wa dharura kuhusu vita vya Wayahudi dhidi ya Gaza?! Je, mkutano wao huu hautakuwa janga kwa watu wa Gaza?! Lau wangekuwa wanaume, wangetumia ujasiri wao kuunga mkono Gaza na watu wake. Na kama wangekuwa na uhusiano na Uislamu, wangetumia sheria zake kukomboa Palestina yote.
Enyi Waislamu: Hamtapata heshima na utu maadamu hawa watu wajinga wanadhibiti hatima yenu na wao ni wafuasi wa Wayahudi na Amerika. Kwa hivyo, majeshi yenu lazima yawaondoe na kutekeleza sheria ya Mungu na kutangaza jihad katika njia ya Mungu, ambayo umma ulipoiacha ulikuwa umedhalilika na ardhi yake na maeneo matakatifu yalitekwa na Wayahudi. Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimshukie, alisema: "Hakuna watu wanaoacha jihad isipokuwa Mungu atawafunika kwa adhabu" na kama Abu Bakr Al-Siddiq, Mungu amridhie, alisema: "Hakuna watu wanaoacha jihad isipokuwa watadhilika."
Imeandikwa kwa Redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Muhammad Salim - Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)