Trump Aingilia Kati Kukomesha Vita dhidi ya Gaza kwa Manufaa ya Amerika na Taasisi ya Kiyahudi
na Sio Kuwanusuru Watu Waliodhulumiwa
Habari:
Rais wa Marekani Trump siku ya Jumapili alitoa wito wa kuharakishwa kwa makubaliano kuhusu Gaza na kurejeshwa kwa mateka wa Kiyahudi wanaoshikiliwa na upinzani wa Palestina. Katika ujumbe wa kushtukiza ambao Trump alichapisha kwenye jukwaa lake la Truth Social, alisema: "Kamilisheni makubaliano kuhusu Gaza na mrejeshe mateka." (Al-Jazeera Net, 29/6/2025, imerekebishwa)
Maoni:
Tangu kuanza kwa vita vya Wayahudi dhidi ya Gaza baada ya shambulio la upinzani wa Palestina dhidi ya taasisi ya Kiyahudi mnamo 7 Oktoba 2023, na licha ya ushujaa ulioandikwa na wapiganaji na uthabiti ulioonyeshwa na watu wa Palestina, na licha ya uhalifu wa Wayahudi dhidi ya raia, haswa watoto na wanawake, hatujasikia sauti yoyote ya serikali ya kimataifa ikitoa wito wa kukomesha mauaji haya, isipokuwa sauti ambazo hazisikiki zikitoa wito wa kukomesha mauaji haya na kuharakisha kufanya makubaliano ya kukomesha vita, lakini tunasikia nchi kubwa ambazo zimeinua kauli mbiu za haki za binadamu, ulinzi wa mtoto na haki za wanawake; zinadai kurejeshwa kwa mateka wa Kiyahudi, kana kwamba watu wa Gaza hawana haki hata ya kuishi!
Wito wa Trump wa kuharakisha makubaliano kuhusu Gaza na kurejesha mateka, unalenga kulinda taasisi ya Kiyahudi na kuimarisha uwepo wake kupitia makubaliano ya usaliti ambayo yanaimarisha mgawanyiko na kukwamisha kile kilichosalia cha upinzani wa kweli.
Tunaishi katika zama ambapo mfumo wa kimataifa uliopo unaporomoka kwa sababu ya udhaifu wake, na tunamiliki mbadala halisi ambayo inaweza kutawala ulimwengu na kueneza haki na huruma ndani yake.
Kwa hivyo ni jukumu letu kutokosa fursa hii, na kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir kuanzisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume na kuwatoa watu kutoka kwenye unyonge na dhuluma ya ubepari kwenda kwenye uadilifu na nuru ya Uislamu.
Mwenyezi Mungu amesema: ﴿WANATAKA KUIZIMA NUR YA ALLAH KWA Vinywa Vyao, NA ALLAH NI MKAMILISHAJI WA NUR YAKE, JAPO WAPENDE WASIO AMINI * YEYE NDIE ALIYEMTUMA MWANZO WAKE KWA UONGOZI NA DINI YA HAKI ILI AITUKUZE JUU YA DINI YOTE, JAPO WAPENDE WASHIRIKINA﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya Idhaa ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Darin Al-Shanti