Kuhalalisha Watawala wa Sham na Entiti ya Kiyahudi
Kuliwahimiza Watawala wa Bahrain Kuanzisha Upya Uhusiano na Wayahudi Baada ya Kukatika
Habari:
Shirika la habari la Bahrain (BNA) lilisema Alhamisi kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Abdul Latif bin Rashid Al-Zayani alipokea jana nakala ya hati za utambulisho za balozi mpya wa Wayahudi nchini Bahrain, Shmuel Revel. Shirika la habari la Bahrain lilisema Al-Zayani alisisitiza katika mkutano wake na balozi "umuhimu wa kuendeleza juhudi zinazochangia kuunga mkono juhudi za amani, usalama na utulivu katika eneo hilo." Ikumbukwe kwamba Bahrain hapo awali ilitangaza kwamba balozi wake kwa entiti ya Kiyahudi alirejea nchini mnamo Novemba 2023 "kwa msaada wa suala la Palestina", na kwamba balozi wa Wayahudi huko Manama aliondoka ufalme. (Al-Jazeera, 28/08/2025 M, imerekebishwa)
Maoni:
Bahrain hapo awali ilikuwa imebadilisha orodha za ugaidi ili kuendana na hali mpya katika eneo hilo, kwani ilimuondoa mhalifu wa maeneo matakatifu, Al-Julani, kutoka kwa orodha hizo kwa ombi la Amerika ili kumtegemea katika kutawala Dameski badala ya Bashar, mteja wake wa zamani, ambayo ni kwamba Amerika ilithibitisha kwamba kupitia watu kama yeye itafanikisha zaidi ya ilivyoota kupitia Bashar.
Na sasa Bahrain inarejesha uhusiano wake na entiti ya Kiyahudi baada ya kuukata kufuatia matukio ya Oktoba 2023 na mauaji na kuzingirwa kwa Waislamu wa Gaza kutokana na hasira inayoongezeka kutoka kwa umma wa Kiislamu.
Watawala wa Bahrain sasa wanarudi kupata kwamba Al-Julani amewatangulia katika kujipendekeza kwa entiti inayokalia na kuonyesha shughuli za uratibu na kuhalalisha licha ya majanga yanayowapata ndugu zetu huko Gaza kutokana na kuzingirwa na mauaji mikononi mwa entiti ya Kiyahudi, bila kujali sheria ya Kiislamu au umma wa Kiislamu.
Lakini kwa hali yoyote, matumaini ya watawala wa Bahrain na watawala wapya wa Sham yamevunjika.
Umma utamfunulia kila msaliti kwa rangi yake halisi, kama rangi ya Dajjal wa Ankara ilivyoonekana baada ya tarehe saba Oktoba 2023 BK. Na ikiwa umma ulifurahi na kukimbia kwa Bashar al-Assad baada ya tarehe nane Desemba 2024 BK, basi una haki ya kufanya hivyo, lakini furaha hii haitalingana na furaha yake siku ambayo kila rangi inaonekana katika uhalisi wake na inafuatiwa na kuanguka kwa viti vya enzi vya watawala wote wa Kiislamu, Waarabu na wasio Waarabu, pamoja na kiti cha enzi cha watawala wapya wa Sham wanaounga mkono Amerika na Uturuki ya kilimwengu, baada ya umma kutekeleza wajibu wake wa kuwawajibisha na kuwaondoa, ili kuishi furaha ya kweli kwa kurejea kwa dola moja ya Kiislamu na umma mmoja wa Kiislamu, na wahubiri wa Uislamu wakizunguka dunia nzima wakisema, "Salimika na utasalimika, Mwenyezi Mungu atakupa thawabu yako mara mbili."
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: ﴿Au wanataka hila? Basi walio kufuru ndio wenye kuhiliwa.﴾.
Imeandikwa kwa ajili ya Radio ya Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Nizar Jamal