«NA IMEFANYWA ARDHI KUWA MSIKITI NA TAHARA KWANGU»
Habari:
Kuzuiliwa kwa wanafunzi wa shule ya upili katika eneo la Hammamet nchini Tunisia kuswali katika uwanja wa shule wakati wa mapumziko kulizua mjadala mkubwa baada ya mkurugenzi wao kuwataka waswali majumbani mwao, akitoa sababu kwamba shule ni mahali pa elimu na sio ibada. Kulingana na video iliyoenea, hali ilizidi na kuwa mabishano ya maneno kati yake na wanafunzi, ambapo mmoja wao alielezea kutoridhika kwake kwa kusema: "Hii ni ardhi ya Mola wangu, na sio ardhi yako wewe!", akisisitiza ushikamano wa wenzake na haki yao ya kufanya ibada ndani ya shule.
Maoni:
Tunisia inasalia kuwa uwanja wa mapambano kati ya ulaikini na harakati za wanawake na kati ya dini, tangu Bourguiba na Ben Ali walipoificha Uislamu kutoka kwa vizazi kimakusudi, na kuifanya kuwa nchi ya kilimwengu inayotawaliwa na sheria za kiraia katika nyanja zote za maisha, hata za kijamii na kielimu. Maagizo yalikuwa yanakataa kuchapisha mada yoyote ya kidini kupitia vyombo vya habari rasmi, ikiwa ni pamoja na kupeperusha sala na adhana kupitia televisheni. Na walikuwa wanakataza wasichana kuvaa hijabu, pamoja na kuzuia kuajiriwa kwa wanawake waliovaa hijabu katika idara rasmi za serikali. Pia, utawala wa Ben Ali ulikataza sala ya jamaa katika misikiti isipokuwa kwa masharti maalum kutoka kwa ujasusi. Na ilikuwa inazuia matumizi ya vipaza sauti kuita adhana. Na vile vile ilikuwa inazuia ndoa za wake wengi hata kama mwanamke hakuzaa, na iliweka vikwazo vikali kwa wale wanaotaka kwenda kutekeleza ibada ya Hija. Na katika ngazi ya elimu, ilizuia uanzishwaji wa shule za kidini na shule za kukariri Quran, pamoja na kuzuia kufundishwa kwa somo la elimu ya Kiislamu katika ngazi zote...
Na baada ya kuondolewa madarakani kwa dhalimu Ben Ali miaka 12 iliyopita, hakuna mengi yaliyobadilika, kwa bahati mbaya, kwa sababu haikuwa mapinduzi yaliyotegemea kutumia sheria ya Mungu duniani, na iliingia katika vita, mizozo na maslahi. Lakini watu wana kiu ya Uislamu na utekelezaji wake, kwani ni dini ya fitra. Na tukio la kukataa wanafunzi kuzuiliwa kuswali ni mfano wa hilo. Tukio hilo lilipata mwingiliano mkubwa, haswa baada ya video kusambazwa kwenye mtandao, ambapo idadi ya wale waliounga mkono msimamo wa wanafunzi ilikuwa kubwa, kwani sala ni faradhi na haki ya kidini ambayo haipaswi kubanwa. Huku wengine wakitoa maoni kwamba mkurugenzi ana haki katika hilo, kwani shule ni mahali pa kujifunza na sio mahali pa ibada na sherehe za kidini, na kwamba mahali pa sala ni msikiti au nyumbani tu! Wengine walisema kwamba ikiwa wanataka kuswali, basi wanapaswa kutaka wizara itenge maeneo kwa ajili hiyo. Shirika la kitaifa la kutetea ustaarabu wa dola lilituma taarifa likizingatia kuwa tukio hili ni hatari sana kwa sababu ya kuchanganya wazi mambo ya kidini, ya kibinafsi na matakatifu, na yale ya kiraia, ya umma na ya kisheria. Na lilisitiza kwamba misikiti na maeneo ya ibada ndio mahali pa asili pa sherehe za kidini, wakati shule inabaki imetengwa pekee kwa ajili ya sayansi na maarifa.
Wanasema upotofu huu wakiwa katika nchi ya Kiislamu na watu wake ni Waislamu na dini yake ni Uislamu ambao ndani yake sala ni nguzo muhimu zaidi na lazima itekelezwe kwa wakati wake katika sehemu yoyote uthibitisho wa kauli yake Mwenyezi Mungu: ﴿Hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekwa wakati maalum﴾. Na anasema Mtume wetu ﷺ: «NA IMEFANYWA ARDHI KUWA MSIKITI NA TAHARA KWANGU», na hakuacha kuitekeleza hata katika vita. Wanakuja hawa wanawazuia wanafunzi kutekeleza faradhi ya sala na wanawaambia waswali majumbani mwao! Na anawaambia Mola Mwenye Enzi: ﴿Ili wachukue mizigo yao kamili Siku ya Kiyama na sehemu ya mizigo ya wale wanaowapoteza bila ya kujua. Hakika ni maovu mno wanayo yabeba!﴾.
Lakini chochote watakachofanya na kujaribu na kutenda, Uislamu utainuka kama ulivyokuwa licha ya pua za makafiri na wasaidizi wao, na licha ya pua za walimwengu na wale waliofuata nyayo zao. Anatutosha Mwenyezi Mungu, naye ni mbora wa wakili.
Nimeiandika kwa ajili ya Radio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Muslima Al-Shami (Um Suhayb)