﴿Na yule ambaye Mwenyezi Mungu anamfedhehesha, basi hana wa kumheshimu﴾
Habari:
Marekani imetangaza kuwanyima maafisa wakuu wa Mamlaka ya Palestina, akiwemo mkuu wao Mahmoud Abbas, visa vya kuingia nchini humo na kufuta visa vya sasa ili kuwazuia kuhudhuria mkutano ujao wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa maoni yake juu ya hatua hii kwa kusema: Utawala wa Trump uko wazi: Ni kwa maslahi ya usalama wetu wa kitaifa kuwawajibisha Shirika la Ukombozi la Palestina na Mamlaka ya Palestina kwa kushindwa kutimiza ahadi zao na kudhoofisha matarajio ya amani. (Al-Jazeera Net - kwa muhtasari, 2025/08/29)
Maoni:
Mamlaka ya Palestina ilisalimisha zaidi ya theluthi mbili ya ardhi ya Palestina huko Oslo ili kuwaridhisha Mayahudi na Amerika, na kisha ikafanya matendo maovu na machafu zaidi ya uratibu wa kiusalama na Mayahudi ambao ulihakikisha kukamatwa, kufuatiliwa na kuuliwa kwa wale wanaopinga uvamizi kutoka kwa watu wa Palestina, kwa tamaa ya radhi ya Mayahudi na wale walio nyuma yao. Ilikuwa na bado ni mkono wa Mayahudi ambao wanatumia kuwakandamiza watu wa Palestina na jicho lake ambalo linafuatilia harakati yoyote dhidi ya uvamizi, na licha ya huduma hizi zote za bure, Amerika na taasisi ya Kiyahudi haziwaridhiki nayo!
Hivi karibuni, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza kuwanyima maafisa wakuu wa Mamlaka ya Palestina, akiwemo Mahmoud Abbas, visa vya kuingia katika ardhi ya Marekani, kwa madai kwamba inaharibu matarajio ya amani na haijatimiza ahadi zake. Hili ni somo kubwa kwa vibaraka wengine ambao bado wanafuata mkondo huo huo ambao Mamlaka ya Dayton kibaraka ilifuata; kwamba Amerika na Mayahudi hawakuheshimu wala kukuona wa muhimu, ninyi si chochote ila watumwa na wahudumu wao ambao mnatimiza amri zao, na kisha Amerika inawageuka bila kujali na kuwatema kama kokwa wala haiwapi zawadi wala shukrani.
Mayahudi hawamwamini mtu yeyote, hata kama atawafanyia huduma zote; adui wa Mwenyezi Mungu, Sisi, ambaye anazingira Gaza na kuwazuia watu wake chakula na maji ili kuwaridhisha Mayahudi, alifanya katika tarehe saba ya mwezi wa Agosti mkataba wa kuagiza gesi kutoka taasisi ya Kiyahudi kwenda Misri kwa thamani ya dola bilioni 35, na ingawa mkataba huu una faida kubwa sana kwa Mayahudi, haukumzuia Netanyahu kutoa tamko baada ya hapo la kutamani kuanzisha (Israel) kubwa ambayo inajumuisha Misri, Syria, Lebanon, Jordan na hata sehemu za Uturuki, laana iwe juu yenu enyi watawala wa Waislamu! Haijalishi mnafanya nini na kutoa huduma gani kwa Mayahudi, hawaoni umuhimu wenu! Siku moja vifaru vyao vitawakanyaga na makombora yao yataangusha viti vyenu vya enzi, na bila shaka hasara yenu itakuwa kubwa wakati huo, kwa sababu wale ambao mmetumia maisha yenu yote kuwahudumia watawaacha ikiwa hawatawaondoa, na watu wenu ambao mmewaonea kwa miongo kadhaa wanasubiri wakati muafaka wa kupindua viti vyenu vya enzi na kuondoa miaka yenu ya ukame ya utawala, na kusimamisha hukumu ya Mwenyezi Mungu katika ardhi, basi subiri, sisi tunasubiri.
Imeandikwa na Idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Muhammad Abu Hisham