Organization Logo

لبنان مكتب

ولاية لبنان

Tel: +961 3 968 140

Fax: +961 70 155148

tahrir.lebanon.2017@gmail.com

Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Lebanon wamtembelea Mhe. Mbunge Dkt. Osama Saad
Press Release

Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Lebanon wamtembelea Mhe. Mbunge Dkt. Osama Saad

October 28, 2025
Location

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir/ Wilaya ya Lebanon

Wamtembelea Mhe. Mbunge Dkt. Osama Saad

Katika kivuli cha mashambulizi ya Kimarekani dhidi ya Lebanon na eneo zima kwa njia ya kuhalalisha uhusiano na kujisalimisha, na juhudi za Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Lebanon za kukabiliana na mashambulizi haya, ujumbe kutoka kwa chama hicho ulifanya ziara siku ya Jumatatu, 2025/10/27, uliowakilishwa na wanachama kutoka kamati ya mawasiliano ya kati na kamati ya shughuli katika eneo la kusini, kwa Mhe. Mbunge Dkt. Osama Saad, katika ofisi yake katika mji wa Saida.

Ujumbe huo ulizungumzia mchakato wa kuhalalisha uhusiano na Kundi la Kiyahudi ambao Marekani inajaribu kulilazimisha Lebanon na eneo zima, na ulazima wa kukabiliana nao, na hili ndilo linalofanywa na Hizb ut-Tahrir, ambapo kufuatia kuanza kwa kampeni yao, vikosi vya usalama vilifanya ukamataji holela wa vijana wake wawili katika mji mkuu Beirut, na kuendelea kuwakamata kwa siku tano bila ya madai yoyote au hati za kukamatwa kisheria!

Mhe. Mbunge alieleza kuwa alikuwa ameashiria mapema mada ya (Amani) katika hotuba yake ya kibunge mbele ya Baraza la Wawakilishi la Lebanon katika alichokiita Amani ya Unyenyekevu baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kusini mwa Lebanon mnamo 2024/11/27, bali imekuwa hivi karibuni Amani ya Unyenyekevu na Utiifu. Mhe. Mbunge alilaani kukamatwa kwa vijana wa chama na mbinu ya kiholela inayotumiwa na mamlaka dhidi ya wale wanaokhalifu maoni yake.

Makubaliano yalikuwa wazi juu ya ulazima wa kuzuia mashambulizi haya ya Kimarekani na Kizayuni ya kuhalalisha uhusiano na Lebanon na eneo zima, na ulazima wa kufanya kazi ya kuwafahamisha watu kupitia semina, mihadhara na kazi za kijamii.

Ujumbe huo ulimshukuru Mhe. Mbunge kwa mapokezi, kwa matumaini ya kuendeleza njia za mawasiliano kati ya Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Lebanon na Mhe. Mbunge.

Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

Katika Wilaya ya Lebanon

Official Statement

لبنان مكتب

ولاية لبنان

لبنان مكتب

Media Contact

لبنان مكتب

Phone: +961 3 968 140

Fax: +961 70 155148

Email: tahrir.lebanon.2017@gmail.com

لبنان مكتب

Tel: +961 3 968 140 | tahrir.lebanon.2017@gmail.com

Fax: +961 70 155148

Reference: PR-019a277f-4ac8-7709-a09a-a7dc44c418e3