Ee Fidan! Ikiwa mko tayari kwa kila dhabihu, basi songeni mbele na jeshi lenu kuelekea Palestina!
Habari:
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, alitoa taarifa baada ya mkutano wa mawaziri kuhusu Gaza uliofanyika Istanbul kwa ushiriki wa mawaziri kutoka Indonesia, Pakistan, Qatar, Saudi Arabia, UAE na Jordan, akisema: "Tuko tayari kutoa kila aina ya dhabihu kwa ajili ya amani." Aliongeza: "Israel inakiuka usitishaji mapigano. Tangu kuanza kwa usitishaji mapigano, karibu Wapalestina 250 wameuawa." (Hurriyat, 2025/11/03)
Maoni:
Hisia za umma zimefifia kuhusu matamko matupu yanayotolewa na watawala vibaraka na watumishi, ambao hawafanyi chochote kwa Wapalestina wala kwa Waislamu, na hawasogezeki hata kidole kimoja kusimamisha mauaji na ukatili dhidi yao! Umma umezowea mikutano yao ambayo ni kama sherehe za chai na kahawa kisha wanaondoka! Umma hautarajii chochote kutoka kwao isipokuwa taarifa hizi tupu! Bali taarifa hii isiyo na maana ya Fidan, aliyoitoa baada ya mkutano wa uhaini, inaonyesha wazi ukubwa wa utata! Anadai kuwa yuko tayari kwa kila dhabihu, na wakati huo huo anakiri kwamba Wayahudi wameua takriban Wapalestina 250 tangu usitishaji mapigano! Hii ni dhabihu gani? Na iko wapi? Ikiwa mko tayari kweli kwa kila dhabihu, kwa nini hamhamishi majeshi yenu dhidi ya chombo cha Kiyahudi kujibu mauaji ya Wapalestina 250 tangu usitishaji mapigano? Hii ni pamoja na wale 67,000 waliouawa hapo awali.
Dhabihu haimaanishi kutoa matamko machache kuhusu Palestina, bali inamaanisha kuvumilia matatizo ambayo yanaweza kusababishwa na kusonga mbele kwa majeshi. Dhabihu si kuhesabu ukiukwaji na idadi ya wahanga, bali ni kubeba matokeo ya mzingiro wa kimataifa kutokana na kutuma majeshi kujibu mauaji ya Waislamu. Dhabihu ya kweli ni kutokaa kimya juu ya dhuluma, bali kuiga matendo ya Mtume ﷺ na Al-Mu'tasim. Dhabihu haimaanishi kutuma vikosi vya kulinda amani kuwalinda Wayahudi na kuimarisha chombo chao, hii si dhabihu, bali ni uhaini wa wazi.
Kwa hivyo, dhabihu ya kweli kwa ajili ya Palestina ni kwa vitendo vinavyoumiza chombo cha Kiyahudi na kuondoa uovu wake. Ama vinginevyo, ni upuuzi mtupu na hauitwi dhabihu. Kwa hivyo ikiwa kweli mnataka kutoa dhabihu kwa ajili ya umma na kwa ajili ya damu ya mashahidi wa Palestina, basi songeni mbele na majeshi yenu mara moja!
Na kwa upande mwingine, mkutano wenu huko Istanbul na maafisa vibaraka wachache kutoka nchi za Kiislamu kupitisha mpango wa usaliti wa Trump, hauthibitishi kamwe kwamba mko tayari kwa kila dhabihu. Katika mikutano isiyo na hesabu kabla ya hii, mmerudia kusema kwamba mko tayari kutoa kila kitu kwa ajili ya Wapalestina lakini hatujaona dhabihu yoyote kutoka kwenu, wala hatua yoyote ya kivitendo, isipokuwa matamko machache mnayoyatoa baada ya mkutano. Mmesahau kwa kujua na kwa makusudi mauaji ya Waislamu 67,000 huko Gaza, na kujeruhiwa kwa mamia ya maelfu. Kwa hivyo, mkutano wenu huko Istanbul haukuwa na lengo la kujadili nini kinaweza kufanywa kwa Palestina, bali kinyume chake; lengo lilikuwa kujadili jinsi ya kulinda chombo cha Kiyahudi na jinsi ya kukiunganisha katika eneo hilo kulingana na mpango mkatili wa Trump. Je, hii si ndiyo lengo la "kikosi cha amani" mnachotaka kutuma?
Inaonekana kwamba dhabihu zenu hazitolewi isipokuwa kwa ajili ya kutekeleza mpango wa usaliti wa Amerika na Trump. Lau mngewapa umma sehemu ya kumi ya kile mlichotoa au mtakachotoa kwa Amerika kama dhabihu, umma ungewakumbatia lakini kwa bahati mbaya, matukio ya Gaza yamethibitisha kwamba ninyi mko upande mmoja, na umma uko upande mwingine kabisa. Na historia ni shahidi mzuri kwamba hakuna na haitakuwepo rejea yoyote itakayotoa dhabihu ya kweli kwa ajili ya umma isipokuwa Ukhalifa. Na bila ya Ukhalifa, Waislamu wataendelea kukabiliana na maumivu makali na majanga katika kila sehemu ya dunia, kwa sababu ya watawala hawa wasaliti wanaotawala vichwa vyao. Leo Gaza, Sudan na Yemen, na Mungu anajua janga litakuwa wapi kesho!
Imeandikwa kwa ajili ya Redio ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir
Arjan Tekin Baş