Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Siku ya Uhuru) ya Sabini na Nane
Pakistan itapata uhuru wake kwa kusimamisha Khilafa Rashidah kwa njia ya Utume
(Imetafsiriwa)
Katika mfumo wa kimataifa uliopo, kinachoitwa uhuru ni mchezo wa kuigiza tu uliopangwa, kwa hivyo ukombozi wa kweli haupatikani isipokuwa serikali inapanga mambo yake ya ndani na uhusiano wake wa nje kulingana na kanuni yake. Watu ambao wanaamini hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu hawataachiliwa kweli isipokuwa watakapotumia mfumo wa Kiislamu katika ardhi yao katika utawala, uchumi, jamii, elimu, na mahakama, pamoja na sera ya kigeni kulingana na Da'wah na Jihad. Hii ndiyo maana halisi ya uhuru; Kwa hivyo Pakistan haijaachiliwa huru bado!
Mtazamo wa haraka katika sera kuu za Pakistan unatosha kuthibitisha hili. Je, sera ya Pakistan kwa Jerusalem na Gaza haijaandaliwa katika Kamandi Kuu ya Marekani, Pentagon, na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani? Je, sera yake kwa Kashmir haijajengwa juu ya kuomba ili kuvutia umakini wa Trump, ingawa tulionyesha kivitendo miezi michache tu iliyopita uwezo wa kuikomboa moja kwa moja? Je, sera ya Pakistan kwa Afghanistan imeundwa na Wizara yetu ya Mambo ya Nje, au na manaibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na viongozi wa kijeshi wa Kamandi Kuu ya Marekani? Je, mawaziri wakuu hawatangazi bila aibu kwamba watatafuta ruhusa kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa ili kupunguza bei za umeme? Je, mahakama za Pakistan bado hazitoi hukumu zao kulingana na sheria ya kawaida ya Kiingereza? Je, mkuu wa jeshi la Pakistan hivi karibuni hakusafiri kwenda Marekani kuhudhuria sherehe ya kustaafu (mkuu wake wa moja kwa moja), Jenerali Corella? Uhuru gani huu, ambapo hatuwezi kuzindua vita kwa ajili ya Kashmir au Gaza, lakini tuko tayari kupigana katika vita vya Marekani?
Pakistan ni mojawapo ya nguvu saba za nyuklia zilizotangazwa ulimwenguni. Tano kati ya nguvu hizi zinadhibiti maeneo tofauti ya ulimwengu na kuunda masuala yake kulingana na masilahi yao wenyewe. Ufaransa na Uingereza zinadhibiti siasa za Ulaya; Marekani inatumia maagizo yake duniani kote; Urusi imejikita katika Ulaya Mashariki; na China inaongeza wigo wa ushawishi wake kwa kasi. Ama taifa la Kihindu, linafanya kazi kwa bidii ili kuwa polisi wa eneo hili. Pakistan inasimama wapi katika mlinganyo huu? Marekani inaweza kufanya mkataba wa nyuklia na Iran na kuufuta, na kuurejesha wakati wowote inapopenda, lakini hatuwezi hata kufanya mkataba wa kununua mafuta na Iran! Kwa nini? Uhuru gani huu?
Enyi Maafisa na askari wa Vikosi vya Wanajeshi vya Pakistan: Kikwazo cha uhuru wa kweli wa Pakistan na ukombozi wake sio ukosefu wa rasilimali, wala ukosefu wa shauku, ujasiri na uwezo wa askari wetu au watu wetu. Mgogoro wetu wa kweli ni uongozi usio na maono, uongozi ambao lazima uondolewe na kubadilishwa na uongozi wa kanuni ambao hupewa ahadi ya ushindi, ili aweze kusimamisha Khilafa Rashidah nchini Pakistan. Hii ndiyo ufafanuzi sahihi wa uhuru wa kweli, na jukumu kubwa la kuutimiza liko juu yenu, na kuongoza Pakistan kufikia lengo hili. Hizb ut-Tahrir imesimama mbele yenu na maono ya kanuni, na inawapa programu na mradi jumuishi. Haya, katika (Siku ya Uhuru) ya sabini na nane, vaeni vazi la uhuru wa kweli, na kataeni mfumo huu wa kimataifa wa ukoloni, na jengeni chini ya bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, mfumo mpya wa kimataifa.
﴿Na hakika hii ndiyo njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutenganisheni na njia yake. Hiyo ndiyo aliyokuusieni, ili mpate kumcha.﴾
Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Katika Wilaya ya Pakistan