July 23, 2025
press_release
Ee, kwa ajili ya ujasiri wa Kiislamu katika umma wa Muhammad ﷺ! Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: «SIYO MWENYE KUAMINI YULE ANALALA ASHIKI NA JIRANI YAKE ANA Njaa PEMBENI YAKE» Imesimuliwa na Al-Hakim Miti na mawe yamenena kutokana na ukubwa wa yaliyotufika; vifua vyetu vinatoa damu na uchungu, watoto wetu wanajikunyata kwa njaa na kiu, wanawake wetu wanaomba msaada.
Miti na mawe yamenena kutokana na ukubwa wa yaliyotufika; vifua vyetu vinatoa damu na uchungu, watoto wetu wanajikunyata kwa njaa na kiu, wanawake wetu wanaomba msaada wa waja wenye imani. Yule asiyekufa kwa makombora atakufa kwa njaa na kiu. Ama uchungu wa kukataliwa ni mbaya zaidi kwetu kuliko makombora, njaa na kiu. Ndugu zenu huko Gaza wanazurura bila makazi, na sauti zao zimekatika kwa udhaifu wa njaa na kiu, baada ya kukata tamaa ya kuokolewa na mtu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, wanaita: Uko wapi umma wa Kiislamu? Uko wapi ujasiri wa dini? Uko wapi msaada wa waumini?