October 13, 2025
Uzbekistan: Risala ya rambirambi kwa mbeba da'wa Mirza Ahmadov Miraziz
Kwa masikitiko makubwa tunamtangazia umma wetu wa Kiislamu mwana mwingine miongoni mwa wana wao wacha Mungu waliosimama imara, na hatumsafishi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ndugu yetu Mirza Ahmad Miraziz amefariki siku ya Ijumaa, Oktoba 10, 2025, na swala ya jeneza iliswaliwa jana, Jumamosi. Miraziz alizaliwa Tashkent mwaka 1970. Alikuwa mmoja wa maelfu ya Waislamu waaminifu na jasiri walioitikia wito wa Hizb ut-Tahrir kwa watu wa Uzbekistan kufanya kazi ya kurejesha maisha ya Kiislamu.