Dunia na mapambo yake na Akhera na neema zake
Anasema Subhaanahu wa Ta'ala: ﴿Jueni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na pambo na majigambo baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo mimea yake huwafurahisha makafiri, kisha hukauka, ukaiona imepauka, kisha inakuwa majani makavu. Na katika Akhera kuna adhabu kali na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na uhai wa dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu﴾, na anasema Subhaanahu wa Ta'ala: ﴿Kukithirisha mali kukakufanyeni msiwe na akili * Mpaka mkayazuru makaburi. * La! Mtakuja jua. * Tena la! Mtakuja jua. * Lau mngeli jua kwa yakini, * Mngeli ona Jahannamu. * Kisha mtaiona kwa jicho la yakini. * Kisha mtaulizwa siku hiyo juu ya neema﴾, Na akasema Ta'ala kuhusu Akhera: ﴿Hakika wema watakuwa katika neema * Na hakika waovu watakuwa Motoni. * Wataingia humo Siku ya Malipo. * Wala hao hawatakuwa wenye kukosekana humo﴾.
Mlinganyo wa ajabu ambao nusu yake inashuhudiwa, inajulikana, inaonekana na inaelezewa ambamo uumbaji wa mwanadamu umo, anaishi nayo usiku na mchana, anaigombania na inamgombania, naye yuko katika hali ya mapambano ya kudumu.
Amesema Ta'ala: ﴿Hakika tumemuumba mwanadamu katika taabu﴾, mwanaadamu huyo anataabika humo usiku na mchana mpaka yakini imjie, naye katika mwendo wake katika uhai wa dunia anaona yakini hii (mauti) inamjia mwingine katika mwendo wake, anaona yakini hii lakini jicho lake liko kwenye pambo na majigambo na wingi, Amesema Ta'ala: ﴿Na mnakula urithi uliochanganyika. * Na mnapenda mali mapenzi ya kupindukia﴾, anaishi na yakini kwa mwingine lakini haihisi ndani ya nafsi yake kabla ya kumjia yakini inamshinda juu ya matamanio yake na kumstusha kabla ya kuipokea, ﴿Basi hakusadiki wala hakisali. * Lakini alikanusha na akageuka﴾... huku ni kughibu kwa basira kunakopata basari gubigubi la kutoufahamu ukweli unaoonekana, unaohisika, unaogusika, siyo ndoto iliyo dhaniwa wala ukweli ulio ghibu, bali ni hali halisi inayogusika, inayo hisika. Lau angeli utambua mwanadamu huyu angeliishi katika dunia yake kwa ukali wake na umaskini wake, na mashaka yake na ubahili wake, na dhiki yake na furaha yake, kwa sababu ameuona maana yake na ameuishi lengo lake, kwa hivyo amejiandaa kwa ajili yake kile anachoamini cha akiba isiyoisha wala kubadilika, rahisi kuibeba nzito katika mizani, ﴿Na tekeni zawadi, kwani bora ya zawadi ni uchamungu. Na nicheni, enyi wenye akili!﴾.
Hu ulinganyo wa dunia unafichua sheria ya kifizikia ya kimaumbile; kwamba chenye thamani na imara na nguvu na chenye kuzaa na chenye kutosheleza ni kile ambacho kinakuwa thabiti hakiyumbishwi wala hakibadiliki wala hakigeuki wala haichukuliwi na upepo, ﴿Kama mti mzuri, ambao mizizi yake ni imara, na matawi yake yako juu; * Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake﴾. Na kwa hivyo ukweli huu wa kifizikia unafichua kanuni kwamba chenye thamani hakionekani wala hakiko juu juu wala hakichukuliwi na upepo, nacho ni kigumu kukigundua na kukifichua kwa sababu kimeingia ndani ya ardhi, mpaka ukifikie unahitaji juhudi na taabu na kujitolea na kutoa na kutaniana kwenye vitabu vya manabii na wanachuoni, kwa sababu ndani ya bahari kuna hazina na mawe ya thamani na juu ya uso wa maji kuna mizoga na povu ﴿Ama povu hupotea bure, na yale yawafaa watu hubaki ardhini. Namna hivi Mwenyezi Mungu hutoa mifano﴾.
Hii inafichua kanuni za uelewa sahihi na uelewa usio sahihi; uelewa sahihi ni ule unaosimama juu ya akida sahihi na akili safi isiyochafuliwa, ambayo inausoma uhalisia ikauchambua kisha inateremsha hukumu ya Mwenyezi Mungu juu yake ima inaihalalisha au inaikataa. Ama uelewa usio sahihi ni uelewa wa juu juu wenye rangi nyingi unaobadilika ambao unachukuliwa na upepo wa matamanio kulia na kushoto hauna jambo thabiti wala ukweli anaouchota, unaelekea kule wanako elekea watu, ni kama povu la bahari linalochukuliwa na upepo na kuelea juu lakini halina faida ikiwa si la kuharibu.
Na katika uhalisia wa kisiasa ambao tunauona na tunaiona sura yake uhalisia ulio pigwa picha hauna doa lolote kwamba wale ambao wameongoza mihrabu na viti na wametawala mpaka shingo zikawatii wao ni povu la bahari na magugu ya nafaka ambayo hayasimami katika mjadala wala uwanja wa ubishi. Wao ni uchafu unaochukuliwa na upepo hawana mizizi wala milima imara. Na hawa ndio wale ambao ametuonya nao Mtume ﷺ kwa sababu ya balaa kubwa na shari iliyoenea wasiozaa na wanafanya uharibifu popote walipoenda na kuondoka, na akasema Ta'ala kuwahusu: ﴿Hao ndio adui, tahadharini nao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wamegeuzwa namna gani!﴾, na akasema ﷺ akionya na akitishia juu ya shari hii ya juu juu inayoonekana wazi na akitishia juu ya balaa lake ambalo litafikia mti na jiwe na binadamu: «Mambo yatakapo pewa wasio waweza, basi ingojeni Saa» yaani ingojeni shari iliyoenea na balaa isiyokuwa na mfano, ambayo milima mirefu inajikinga nayo na hazina katika maficho yake na samaki wa baharini wanaomba ulinzi kutokana na shari yake na kwa hili akasema Mwenyezi Mungu Ta'ala: ﴿Ufisadi umefika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale ambayo mikono ya watu imeyachuma﴾ na akasema ﷺ: «Makundi mawili ya watu yakiwa mazuri, watu watakuwa wazuri, na yakiwa mabaya, watu watakuwa wabaya: Wanachuoni na Viongozi» na watu hapa si watu wote bali watu katika riwaya mbili ni makundi mawili ambayo ameyabainisha Mtume Mtukufu ﷺ.
Imeandikwa kwa ajili ya idhaa ya Ofisi ya Habari Kuu ya Hizb ut Tahrir
Salim Abu Subaitan