Tafakuri katika kitabu: "Miongoni mwa vipengele vya Saikolojia ya Kiislamu" - Kipindi cha kumi na nane
Tafakuri katika kitabu: "Miongoni mwa vipengele vya Saikolojia ya Kiislamu" - Kipindi cha kumi na nane

AlhamduliLlah, Mola Mlezi wa walimwengu, na sala na salamu zimwendee imamu wa wachamungu, na bwana wa mitume, aliyetumwa kama rehema kwa walimwengu, Bwana wetu Muhammad na ahli zake na masahaba zake wote, na tujaalie kuwa pamoja nao, na tukusanye katika kundi lao kwa rehema yako, Ewe Mwingi wa rehema kuliko wote wenye rehema.

0:00 0:00
Speed:
November 17, 2025

Tafakuri katika kitabu: "Miongoni mwa vipengele vya Saikolojia ya Kiislamu" - Kipindi cha kumi na nane

Tafakuri katika kitabu: "Miongoni mwa vipengele vya Saikolojia ya Kiislamu"

Maandalizi ya Ustadhi Muhammad Ahmad Al-Nadi

Kipindi cha kumi na nane

AlhamduliLlah, Mola Mlezi wa walimwengu, na sala na salamu zimwendee imamu wa wachamungu, na bwana wa mitume, aliyetumwa kama rehema kwa walimwengu, Bwana wetu Muhammad na ahli zake na masahaba zake wote, na tujaalie kuwa pamoja nao, na tukusanye katika kundi lao kwa rehema yako, Ewe Mwingi wa rehema kuliko wote wenye rehema.

Wasikilizaji wapenzi, wasikilizaji wa redio ya Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir:

Assalamu alaikum warahmatullahi wabarakatuh, na baada ya hayo: Katika kipindi hichi tunaendelea na tafakuri zetu katika kitabu: "Miongoni mwa vipengele vya Saikolojia ya Kiislamu". Na kwa ajili ya kujenga utu wa Kiislamu, pamoja na kuzingatia akili ya Kiislamu na saikolojia ya Kiislamu, tunasema na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu:

Kumcha Mwenyezi Mungu kwa siri na dhahiri ni faradhi, na dalili ya hilo ni Kitabu na Sunna. Ama Kitabu ni kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na mimi nicheni}. (Al-Baqara 40). Na kauli yake: {Na mimi ogopeni}. (Al-Baqara 41). Na kauli yake: {Hakika huyo ni shetani anawatia khofu rafiki zake; basi msiwaogope, bali niogopeni mimi, ikiwa nyinyi ni Waumini}. (Al-Imran 175). Na kauli yake: {Na Mwenyezi Mungu anakuonyeni (mateso yake). Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu}. (Al-Imran 28). Na kauli yake: {Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi}. (Al-Maida 3). Na kauli yake: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu}. (An-Nisa 1). Na kauli yake: {Hakika Waumini ni wale ambao Mwenyezi Mungu anapo tajwa nyoyo zao hujaa khofu}. (Al-Anfal 2). Na kauli yake: {Na hivi ndivyo inavyokuwa kushika kwa Mola wako Mlezi anapo zishika nchi zilizo dhulumu. Hakika kushika kwake ni kuumiza, ni kukali. Hakika katika haya kuna mazingatio kwa anaye ogopa adhabu ya Akhera. Hiyo ni Siku itayo kusanyiwa watu, na hiyo ni Siku itayo hudhuriwa. Nasi hatuiakhirishi ila kwa muda maalumu. Siku itakayo kuja, nafsi haitasema ila kwa idhini yake. Basi wapo watakao kuwa na shari na watakao kuwa na heri. Ama wale walio kuwa na shari basi wataingia Motoni, humo watakuwa na kulia na kupiga chafya}. (Hud 106). Na kauli yake: {Na ambao huunganisha alivyo amrisha Mwenyezi Mungu kuunganishwa, na wanamwogopa Mola wao Mlezi, na wanaikhofu hesabu mbaya}. (Ar-Ra'd 21). Na kauli yake: {Hayo ni kwa anaye ogopa kusimama mbele yangu na akaogopa ahadi yangu}. (Ibrahim 14). Na kauli yake: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Saa ni jambo kubwa. Siku mtakayo iona kila mwanamke mwenye kunyonyesha atasahau alicho nyonyesha, na kila mwanamke mwenye mimba ataondoa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, lakini hawakulewa, lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali}. (Al-Hajj 2). Na kauli yake: {Na kwa anaye ogopa kusimama mbele ya Mola wake Mlezi zipo Bustani mbili}. (Ar-Rahman 46). Na kauli yake: {Mna nini hamumtarajii Mwenyezi Mungu kuwa Mkuu?}. (Nuh 13) Na maana yake ni mbona hamuogopi utukufu wa Mwenyezi Mungu. Na kauli yake: {Siku mtu atakapo mkimbia ndugu yake, Na mama yake na baba yake, Na mkewe na watoto wake. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na mambo yake yanayomshughulisha}. ('Abasa 37).

Ama Sunna na Athari, zipo zenye kuonyesha kwa matamshi yake ulazima wa kuogopa na zipo zenye kuonyesha kwa maana yake:

Imepokewa na Bukhari kutoka kwa Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم alisema: "Watu saba Allah Ta'ala atawavika kivuli chake siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli chake: Imamu mwadilifu, na kijana aliyekulia katika ibada ya Allah Mwenyezi na Mtukufu, na mtu ambaye moyo wake unaning'inia katika misikiti, na watu wawili walio pendana kwa ajili ya Allah, walikutana kwa ajili yake, na wakaachana kwa ajili yake, na mtu aliyefuatwa na mwanamke mwenye cheo na uzuri akasema: Mimi namcha Allah, na mtu aliyetoa sadaka akaificha mpaka mkono wake wa kushoto haujui kile kinachotolewa na mkono wake wa kulia, na mtu aliyemkumbuka Allah akiwa peke yake yakamtoka machozi".

Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم alihutubu hotuba, sijasikia mfano wake kabisa akasema: "Lau mngejua ninayoyajua mngecheka kidogo na mngelia sana" masahaba wa Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم walifunika nyuso zao kwa sauti ya chini ya kulia. (Wamekubaliana).

Na kutoka kwa Adiy bin Hatim Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم alisema: "Hakuna hata mmoja wenu isipokuwa Allah atazungumza naye, hakuna mkalimani kati ya Allah na yeye, basi ataangalia upande wake wa kulia na hataona isipokuwa aliyoyatanguliza, na ataangalia upande wake wa kushoto na hataona isipokuwa aliyoyatanguliza, na ataangalia mbele yake na hataona isipokuwa moto umemuelekea usoni, basi uogopeni moto hata kama ni kwa kipande cha tende". (Wamekubaliana).

Na kutoka kwa Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: Nilimsikia Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم akisema: "Watu watakusanywa siku ya kiyama wakiwa hawana viatu, wamevua nguo, hawajatahiriwa, nikasema ewe Mtume wa Allah wanaume na wanawake wote wataangaliana? Akasema ewe Aisha jambo ni kubwa zaidi kuliko kuwashughulisha na hilo" (Wamekubaliana).

Na kutoka kwa Nu'man bin Bashir Radhi za Allah ziwe juu yao alisema: "Nilimsikia Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم akisema: "Hakika wepesi wa watu wa motoni adhabu siku ya kiyama ni kwa mtu ambaye atawekwa chini ya nyayo zake makaa mawili ya moto ambayo ubongo wake utachemka kutokana nayo". (Wamekubaliana).

Na kutoka kwa Abdullah bin Umar, Radhi za Allah ziwe juu yao kwamba Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم alisema: "Siku watu watakaposimama kwa ajili ya Mola Mlezi wa walimwengu, mpaka mmoja wao atazama katika jasho lake hadi nusu ya masikio yake".

Na kutoka kwa Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم alisema: "Watu watatoa jasho siku ya kiyama mpaka jasho lao litakwenda ardhini dhiraa sabini, na litawafunika mpaka litafika masikioni mwao". (Wamekubaliana).

Na kutoka kwa Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم alisema: "Allah anasema ikiwa mja wangu anataka kufanya uovu basi msiuandike mpaka aufanye, akisha ufanya basi uandikeni kama ulivyo, na ikiwa ameuacha kwa ajili yangu basi mwandikieni jema, na ikiwa anataka kufanya jema na hakulifanya basi mwandikieni jema, akisha lifanya basi mwandikieni mara kumi yake mpaka mara mia saba". (Wamekubaliana). Je, kwa nini hatumchi Allah kwa siri na dhahiri kama vile masahaba Radhi za Allah ziwe juu yao walikuwa wanamcha, na hilo likawasukuma kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake ili tufanikiwe kama walivyofanikiwa duniani na akhera?

Wasikilizaji wapenzi: Wasikilizaji wa redio ya Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir:

Tunatosheka na kiasi hichi katika kipindi hichi, kwa kuwa tutakamilisha tafakuri zetu katika vipindi vijavyo InshaAllah Taala, mpaka wakati huo na mpaka tutakapokutana tena, tunawaacha katika uangalizi wa Allah na hifadhi yake na amani yake. Tunawashukuru kwa usikilizaji wenu mzuri na Assalamu alaikum warahmatullahi wabarakatuh.

More from Sauti na Video