Machapisho ya Hivi Karibuni

Makala Iliyoangaziwa

null

null

Soma zaidi
Watoto Wanakufa kwa Njaa... Na Watawala Wanaendelea Kuteleza!

Watoto Wanakufa kwa Njaa... Na Watawala Wanaendelea Kuteleza!

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza, Dk. Munir al-Barsh, amefichua kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaokufa kwa njaa, akisisitiza kwamba uvamizi "unafurahia kuwaua," huku mzingiro na kufungwa kwa vivuko vikiendelea na mfumo wa kimataifa ukipuuza. Katika mahojiano kupitia kituo cha Al Jazeera, Al-Barsh alisema kuwa idadi ya watoto ambao wameuawa kutokana na utapiamlo mkali imefikia 66 hadi sasa, wa mwisho wao akiwa mtoto Jouri Al-Masry, mwenye umri wa miezi 3, akionyesha kuwa makundi hatarishi zaidi, haswa watoto, wamekuwa mstari wa mbele wa wahasiriwa.

Jarida la Ar-Raya: Jibu la Swali: Uchokozi wa Taasisi ya Kiyahudi dhidi ya Iran na Matokeo yake

Jarida la Ar-Raya: Jibu la Swali: Uchokozi wa Taasisi ya Kiyahudi dhidi ya Iran na Matokeo yake

Al-Arabiya ilichapisha kwenye tovuti yake mnamo 2025/6/27: (Vyanzo 4 vya kuaminika vilisema kuwa utawala wa Rais Donald Trump ulijadili uwezekano wa kuisaidia Iran kupata hadi dola bilioni 30 ili kujenga mpango wa nyuklia wa kuzalisha nishati kwa madhumuni ya kiraia. Vyanzo viliongeza kuwa mazungumzo haya yaliendelea wiki hii baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kufikiwa. Maafisa wa utawala wa Trump walithibitisha kuwasilisha mapendekezo kadhaa, ambayo ni mapendekezo ya awali na yaliyokuzwa na kipengele kimoja kisichobadilika ambacho hakiwezi kujadiliwa ambacho ni "kusimamisha kabisa urutubishaji wa uranium wa Iran").

Jarida la Ar-Raya: Kushindwa kwa Umoja wa Ulaya katika Kupitia Mkataba wa Ushirikiano na Taasisi ya Kiyahudi

Jarida la Ar-Raya: Kushindwa kwa Umoja wa Ulaya katika Kupitia Mkataba wa Ushirikiano na Taasisi ya Kiyahudi

Umoja wa Ulaya ulitoa ripoti mnamo Juni 20 iliyopita ambayo ililaani taasisi ya Kiyahudi kwa sababu ya uchokozi wake dhidi ya Gaza, na ilijumuisha hitimisho ambalo lilitajwa kuwa hatari, na likaainishwa kama (ukiukaji unaowezekana) uliofanywa na taasisi ya Kiyahudi dhidi ya Wapalestina, na kusababisha kuathiriwa kwa haki za binadamu katika Ukanda wa Gaza, jambo ambalo linapingana na masharti ya Kifungu cha Pili cha Mkataba wa Ushirikiano wa Ulaya na Wayahudi.

Jarida la Ar-Raya: Yanayojiri katika Vita vya Sudan

Jarida la Ar-Raya: Yanayojiri katika Vita vya Sudan

Baraza la Usalama lilifanya kikao kuhusu Sudan katika makao yake makuu mjini New York siku ya Ijumaa tarehe 27 Juni/Juni 2025 BK, na hotuba ya Katibu Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Afrika Martha Pobee ilisema: (Wiki iliyopita, Baraza la Usalama liliwasikiliza wenzetu katika uwanja wa kibinadamu kuhusu hali mbaya. Tunatafuta usitishaji mapigano wa kibinadamu unaotarajiwa na uliowekwa muda ili kuwezesha harakati salama za misaada ya kibinadamu kwenda na kutoka maeneo yaliyoathiriwa na mapigano yanayoendelea, kuanzia El Fasher, na kuruhusu raia kuondoka kwa hiari na kwa usalama.

246 / 10603