Jarida la Ar-Raya: Wazungu hutufurahisha kwa midomo yao lakini mioyo yao na mikono yao hukataa isipokuwa kuwasaidia Wayahudi
Hakuna shaka kwamba uwanja wa kimataifa umeshuhudia mabadiliko makubwa kuhusiana na maoni ya umma wa kimataifa kuhusu vita vya Wayahudi dhidi ya Ukanda wa Gaza. Miezi mirefu ya vita, ambayo imeongezeka na kuwa zaidi ya miezi 20 hadi sasa, imefichua ukatili na uhalifu usio na kifani uliofanywa na uvamizi katika picha zake mbaya zaidi dhidi ya watoto, wanawake, wazee, majengo, hospitali, vituo vya malazi, shule na alama zote za maisha ya kibinadamu, hadi kufikia hatua ambayo ilifichua kila lililofichika, na kuondoa simulizi ya Wayahudi na dhuluma ambayo wamekuwa wakieneza wao na viongozi wa Magharibi mbele ya watu wao.