Kuvuliwa Silaha kwa Hizbullah wa Iran na Jukumu la Mamlaka ya Lebanon!
Makubaliano ya kusitisha mapigano ya tarehe 27 Novemba 2024 BK kati ya chombo cha Kiyahudi na Mamlaka ya Lebanon chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Marekani, yameweka msingi wa kisiasa wa kuvuliwa silaha kwa Hizbullah wa Iran na silaha nyinginezo za makundi ya Kipalestina nchini Lebanon, si kwa sababu ya kupenda "amani" kutoka Marekani, bali kuhakikisha usalama wa chombo cha Kiyahudi ili kuandaa kutokomezwa kwa chochote kilichosalia cha uwezo mdogo wa Waislamu kupigana nao, haswa baada ya matukio ya kimbunga cha Al-Aqsa... Makubaliano haya ni sehemu ya mpango mkuu wa usalama unaoongozwa na Marekani ili kurekebisha mdundo