Neno la Msemaji Rasmi wa Hizb ut-Tahrir katika Wilaya ya Sudan Katika Mkutano na Waandishi wa Habari Siku ya Jumamosi 22 Safar 1447 Hijria, Inayolingana na 2025/08/16 Miladia, yenye kichwa: "Wito kwa Watu wa Sudan.. Iokoeni Darfur Isije Ikaungana na Kusini"
Majeshi ya Msaada wa Haraka yalitangaza siku ya Jumamosi 2025/07/26 Miladia, kuunda serikali sambamba na serikali iliyopo Sudan, katika mji mkuu wa Darfur Kusini (Nyala), na hatua hii ya Majeshi ya Msaada wa Haraka, ni hatua ya kimaendeleo katika kutenganisha eneo la Darfur, ambalo wanalidhibiti, isipokuwa sehemu za mji wa Al-Fasher, ambao wameuwekea mzingiro mkali kwa zaidi ya mwaka mmoja, na wanafanya mashambulizi ya mara kwa mara ili kuuangusha, ili eneo lote la Darfur liwe chini ya udhibiti wao.