NAFASI ZA MATUNDA
Ukweli wa Toba
Basi hakika (Toba) ni kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa kuzingatia kufanya anayopenda na kuacha anayochukia, basi ni kurejea kutoka katika machukizo kwenda kwenye mapenzi, basi kurejea kwenye mapenzi ni sehemu ya jina lake na kurejea kutoka kwenye machukizo ni sehemu nyingine, na kwa ajili ya hili amefungamanisha Subhaanahu mafanikio kamili na kutenda yaliyoamrishwa na kuacha yaliyokatazwa nayo, akasema: {NA TUBUNI KWA MWENYEZI MUNGU NYOTE ENYI WAUMINI, ILI MPATE KUFANIKIWA} Basi kila mwenye kutubu amefanikiwa, na hawi mwenye kufanikiwa isipokuwa yule aliyetenda aliyoamrishwa na kuacha aliyokatazwa nayo. Na akasema Ta'ala: {NA WASIOTUBU, BASI HAO NDIO MADHALIMU} Na anayeacha aliyoamrishwa ni dhalimu kama vile anayetenda aliyokatazwa ni dhalimu, na kuondoka jina la (dhulma) kwake ni pale tu itakapokuwa Toba imejumuisha mambo mawili. Basi watu ni mafungu mawili: Mwenye kutubu na dhalimu, hakuna kingine. Basi wenye kutubu ndio {WAABUDUO, WENYE KUMHIMIDI, WASAFIRIO, WARUKUA'O, WASUJUDUO, WAAMRISHAO MEMA NA WAKATAZAO MABAYA, NA WAHIFADHI WA MIPAKA YA MWENYEZI MUNGU} Basi kuhifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu: ni sehemu ya Toba, na Toba ni jumla ya mambo haya, na ameitwa mwenye kutubu: kwa sababu ya kurejea kwake kwenye amri ya Mwenyezi Mungu kutoka kwenye makatazo yake, na kwenye utiifu wake kutoka kwenye maasi yake.
Madaarij As-Saalikiin Juzuu ya Tatu
Na umshushie rehema Mola wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba wake wote
Na Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh