NAFISI ZA MATUNDA
Changanyikeni na jitengeni
Alisema Al-Hasan Al-Basri, Mwenyezi Mungu amrehemu: Amesema Umar bin Al-Khattab, Mwenyezi Mungu amridhie: Changanyikeni na jitengeni
Kisha anasema Al-Hasan: Changanyikeni na watu katika tabia njema, na jitengeni nao katika matendo machafu.
Adabu za Al-Hasan Al-Basri, kujinyima kwake dunia na mawaidha yake
Na Abu al-Faraj Ibn al-Jawzi
Mola wasalia juu ya Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Amani iwe juu yenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake