Vito vya Thamarati - Ikiwa Mwenyezi Mungu atakunusuruni, basi hakuna atakayewashinda
Vito vya Thamarati - Ikiwa Mwenyezi Mungu atakunusuruni, basi hakuna atakayewashinda

Enyi majeshi katika nchi za Kiislamu: Hakika historia daima hujirudia, na nyinyi mtakapouhami Uislamu kwa kumtii Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta'ala, mtapata nusra ya Mwenyezi Mungu kwenu, kama alivyowanusuru Subhaanahu wa Ta'ala viongozi wa kijeshi Waislamu waliowatangulia, wakawashinda maadui zao licha ya matatizo waliyokuwa wakikabiliana nayo (kama vile kiongozi Khalid bin Al-Walid, Salahuddin, na Muhammad bin Al-Qasim...)

0:00 0:00
Speed:
June 15, 2025

Vito vya Thamarati - Ikiwa Mwenyezi Mungu atakunusuruni, basi hakuna atakayewashinda

Vito vya Thamarati

Ikiwa Mwenyezi Mungu atakunusuruni, basi hakuna atakayewashinda

Enyi majeshi katika nchi za Kiislamu: Hakika historia daima hujirudia, na nyinyi mtakapouhami Uislamu kwa kumtii Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta'ala, mtapata nusra ya Mwenyezi Mungu kwenu, kama alivyowanusuru Subhaanahu wa Ta'ala viongozi wa kijeshi Waislamu waliowatangulia, wakawashinda maadui zao licha ya matatizo waliyokuwa wakikabiliana nayo (kama vile kiongozi Khalid bin Al-Walid, Salahuddin, na Muhammad bin Al-Qasim...), basi sasa endeleeni katika nyayo za hawa viongozi wa kijeshi wema, na mtoe nusra kwa ajili ya kusimamisha Khilafa kwa manhaj ya Utume, na hamtakuwa na haja ya nusra ya yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta'ala nanyi mkiwa katika njia ya ushindi, Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta'ala: ﴿Ikiwa Mwenyezi Mungu atakunusuruni, basi hakuna atakayewashinda, na ikiwa atakuachilieni, ni nani basi atakayekunusuruni baada yake? Na kwa Mwenyezi Mungu wategemee Waumini﴾.

Mwenyezi Mungu amfikishie rehema Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba wake wote

Na Amani iwe juu yenu na Rahma ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake

More from null

Thamani za Matunda - Ni haki kwa yule anayejua kwamba mauti ndio mahali pake pa kuelekea

Thmani za Matunda

Ni haki kwa yule anayejua kwamba mauti ndio mahali pake pa kuelekea

Alisema Al-Hasan Al-Basri, Mwenyezi Mungu amrehemu: Ni haki kwa yule anayejua kwamba mauti ndio mahali pake pa kuelekea, na Kiyama ndio ahadi yake, na kusimama mbele ya Mwenye Nguvu, ndio mahali pake pa kushuhudia, huzuni yake iwe ndefu duniani, na hamu yake iwe katika matendo mema. 

Adabu za Al-Hasan Al-Basri, kujiepusha kwake na dunia na mawaidha yake

Na Abu al-Faraj Ibn al-Jawzi

Mwenyezi Mungu amfikishie rehema Bwana wetu Muhammad na ahli zake na masahaba zake wote

Na Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake

Zawadi Bora - Kukamilisha Kazi Mara Moja

Zawadi Bora

Kukamilisha Kazi Mara Moja

Miongoni mwa mambo yenye manufaa ni kukamilisha kazi mara moja, na kuwa na muda wa ziada katika siku zijazo kwa sababu kazi zisipokamilishwa, mabaki ya kazi zilizopita yatakusanyika, na kazi za baadaye zitaongezeka, na uzito wake utaongezeka, lakini ukikamilisha kila kitu kwa wakati wake, utafanya mambo yajayo kwa nguvu ya mawazo na nguvu ya kazi. 

Njia za Kufurahia Maisha kwa Furaha

Na Ibn Saadi

Mwenyezi Mungu amfikishie rehema Bwana wetu Muhammad, ahli zake na masahaba zake wote

Na Amani iwe juu yenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake