NAFASI ZA THAMANI
MTUME WA ALLAH HAKUKUWA AKIONDOKA KATIKA MAJLIISI YAKE ISIPOKUWA ALIOMBA DUA HIZI
Alituhadithia Yahya bin Ayubu kutoka kwa Ubaidillah bin Zahri kutoka kwa Khalid bin Abi Imran kwamba Ibn Umar alisema: Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم hakukua akiondoka katika majlisi yake isipokuwa aliomba dua hizi Ee Mwenyezi Mungu, tugawie khofu yako itakayotutenga baina yetu na maasi yako, na utiifu wako utakaotufikisha kwenye rehema yako, na yakini itakayoturahisishia misiba ya dunia, na utufurahishe kwa masikio yetu na macho yetu na nguvu zetu maadamu umetuhuisha, na ujaalie kuwa ndio mrithi wetu, na ujaalie kisasi chetu kiwe kwa aliyetudhulumu, na utunusuru juu ya aliyetufanyia uadui, wala usijaalie msiba wetu uwe katika dini yetu, wala usijaalie dunia iwe ndio hamu yetu kubwa, wala upeo wa elimu yetu, wala usitawalishe juu yetu asiyeturehemu.
ZUHUDU NA RAQAIQ
Kwa Abu Abd Rahman Abd Allah bin Al-Mubarak
Na umsalie Ee Mwenyezi Mungu Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba wake wote
Na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh