Vito Vizuri vya Matunda
Kila Mfu Hufungwa Amali Zake
Kutoka kwa Fadhalah bin Ubaid (Radhi za Allah ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume wa Allah ( صلى الله عليه وسلم ) kwamba alisema: "Kila mfu hufungwa amali zake, isipokuwa yule aliyefariki akilinda mpaka katika njia ya Allah, kwani huongezewa amali zake mpaka Siku ya Kiyama, na huaminika na fitna ya kaburi" Imepokewa na Tirmidhi na akasema ni hadithi nzuri sahihi
Mwenyezi Mungu umsalie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Amani iwe juu yenu pamoja na Rahma na Baraka za Mwenyezi Mungu