NAFĀ'ISU ATH-THAMARĀTI
MAN ANFAQA nafaqatan fāḍilatan
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: «Mwenye kutoa sadaka ya ziada katika njia ya Mwenyezi Mungu basi ni mia saba, na mwenye kutoa kwa nafsi yake na familia yake au kumtembelea mgonjwa au kuondoa madhara basi jema moja ni kwa mfano wake kumi, na funga ni ngao madamu haijaivunja, na mwenye kujaribiwa na Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla kwa mtihani katika mwili wake basi ni kwake msamaha»
Ameipokea Ahmad
Mwenyezi Mungu awarehemu Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Amani iwe juu yenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake