Vito vya Matunda
Mawaidha katika Kuhisabu Nafsi
Imesemekana kwamba mtu aliketi kwa hakimu wa Basra "Iyas bin Muadh Al-Muzni"
Mtu huyu alimsengenya ndugu yake katika baraza la Iyas ...
Iyas akamgeukia akisema: "Ewe mtu .. Je, umepigana vita na Warumi?
Akasema: Hapana!
Iyas akasema: Je, umepigana vita na Sind?
Mtu akasema: Hapana!
Iyas akasema: Je, umepigana vita na Watuki?
Mtu akasema: La Hasha!
Iyas akasema: Subhanallah ... Wote hawa wameokoka kutoka kwako na ndugu yako hajaokoka kutoka kwenye ulimi wako".
Ewe Mola, tahirisha majalisi yetu kutoka kusema lile linalokuudhi, na utuepushe kusema yale yasiyo tuhusu, na uturuzuku kusema yale yanayokuridhisha kutoka kwetu.
Na sali Ewe Mola juu ya Bwana wetu Muhammad na familia yake na masahaba zake wote
Na amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake