NAFÂISI ATH-THAMARÂTI
WATU WATATU ALLAH ANA HAKI YA KUWASAIDIA
Kutoka kwa Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Allah ﷺ: (Watu watatu Allah ana haki ya kuwasaidia: Mpiganaji jihadi katika njia ya Allah, na mwandishi anayetaka kulipa deni lake, na anayeoa ambaye anataka kujisitiri).
Imepokewa na Tirmidhiy
Mola wangu mpe rehema Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na amani iwe juu yenu na Rehema za Allah na Baraka zake