NAFASI ZA MATUNDA
NA USHINDI UMETOKA KWA ALLAH TU
Enyi Waislamu: Hakika Waislamu, wanazuoni, na harakati za Kiislamu wanapaswa kukusudia kumtegemea Allah pekee, na wajiharamishie kile ambacho Allah Mtukufu amewaharamishia cha kutafuta msaada kutoka kwa Magharibi ya kibepari kafiri, na tunatangaza mbele ya Allah tukitafuta radhi yake, na mbele ya Umma wa Kiislamu kwamba tunautaka na tunajitahidi kuusimamisha na tunautangaza kuwa ni kwa ajili ya Allah pekee: «Ukhalifa ulioongoka kwa manhaj ya Utume», kwani ni ahadi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliposema: «Kisha kutakuwa na Ukhalifa ulioongoka kwa manhaj ya Utume». Na hakika ni heshima kwetu kuwa wa kwanza kuulingania, kwani kama alivyotaja Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni dalili ya mwisho wa utawala wa kidhalimu ambao sote tunashuhudia kipindi cha mwisho wake, na hili ndilo linalotufanya tusonge mbele zaidi na zaidi katika njia hii.
Naam, anayetaka kusimamisha Ukhalifa ulioongoka anapaswa kumuamini Allah pekee, na asitafute msaada ila kutoka kwake, na asimuogope ila Allah Mtukufu, asimuogope Amerika, wala Ulaya, wala yeyote ila Allah pekee... Na anayetaka ushindi, basi ushindi unatoka kwa Allah تعالى, amesema تعالى: {NA USHINDI UMETOKA KWA ALLAH TU} [Al-Anfal 10] na kwa hivyo tunamuomba Yeye Mtukufu, na tunajua kwamba hatoi ila kwa yule aliyemsaidia, amesema تعالى: {IKIWA MTAMSAIDIA ALLAH, ATAWASAIDIA NA ATAITHIBITISHA MIIGUU YENU}
NA UMSALIE EE ALLAH JUU YA BWANA WETU MUHAMMAD NA JUU YA FAMILIA YAKE NA MASWAHABA WAKE WOTE
NA AMANI IWE JUU YENU NA REHEMA ZA ALLAH NA BARAKA ZAKE