Nafais Althamarati
Kukataza Dhana Mbaya
Amesema Allah Mtukufu: {Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi. Hakika baadhi ya dhana ni dhambi} Al-Hujurat
Na kutoka kwa Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake, kwamba Mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم amesema: "Tahadharini na dhana, kwani dhana ni uongo mkubwa wa hadithi". Imekubaliwa
Mola wetu mjalie rehema Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Amani iwe juu yenu pamoja na Rehema za Allah na Baraka zake